KAMANDA
wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Willbroad Mutafungwa amesema
kuwa, uwepo wa Mahakama ya Watoto ya Ukiukaji wa Makosa ya Barabarani
unasaidia kwa kiwango kikubwa kupunga ajali zisizokuwa za lazima.
Mmoja
ya madereva akisoma kiapo cha ahadi ya kutorudia kuvunja sheria za
Usalama Barabarani baada ya kutakiwa kufanya hivyo wakati wa uendeshaji
na kesi ya madereva waliokamatwa kwa kuvunja Sheria za Usalama
Barabarani katika Mahakama ya Watoto.Mahakama hiyo imeendeshwa na
wanafunzi wa Shule ya Msingi Olimpio mkoani Dar es Salaam ikiwa ni
sehemu ya utoaji elimu kwa wananchi kuzingatia sheria ili kupunguza
ajali.Wa kwanza kushoto aliyekaa na wanafunzi hao ni Kamanda wa Jeshi la
Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Wilbroad Mutafungwa ambaye
alikuwa akifuatilia namna wanafunzi hao wanaovyosikiliza kesi na kutoa
hukumu kwa madereva. (DIRAMAKINI).
Mutafungwa
ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akishuhudia uendeshwaji wa
Mahakama hiyo na kusomewa mashtaka pamoja na kupewa hukumu kwa baadhi ya
madereva waliokuwa wakifanya makosa na kufikishwa kwenye chumba maalumu
katika Shule ya Msingi Olimpio iliyopo Upanga wilayani Ilala.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Wilbroad Mutafungwa
(katikati) akiwa na maofisa wa Jeshi hilo pamoja na Mkurugenzi wa
Shirika la Amend Tanzania, Simon Kalolo ( wa tatu Kushoto) na Meneja
Programu, Neema Swai (wa kwanza kushoto). (DIRAMAKINI).
Amesema kuwa, Mahakama hiyo inaleta msaada mkubwa katika jamii na
hasa katika kuondosha au kupunguza uwepo wa Makosa ya barabarani kwa
madereva ambao wanashindwa kufuata sheria za barabarani zilizowekwa na
mamlaka husika.
"Leo nimekuja kushudia hapa mimi mwenyewe
uendeshaji wa Mahakama hii ya watoto kwa kweli watoto hawa wana uwezo
mkubwa sana, embu fikiria wanakuuliza maswali mtu mzima na unatoa ahadi
na kiapo cha kutorudia makosa, jambo hili ni zuri na sisi kama Jeshi la
Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani tutaendelea kutoa
ushirikiano mkubwa kwa shirika hili la Amend."amesema Kamanda
Mutafungwa.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Wilbroad Mutafungwa
(katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wa Shule ya
Msingi Olimpio mkoani Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Shirika la Amend
Tanzania, Simon Kalolo ( wa pili kushoto),maofisa wa Polisi Kikosi cha
Usalama Barabarani pamoja na wanafunzi wa shule hiyo. (DIRAMAKINI).
Wanafunzi
wa Shule ya Msingi Olimpio mkoani Dar es Salaam ambao waliokuwa
wakiendesha kesi katika Mahakama ya Watoto kwa kusikiliza na kutoa
hukumu kwa madereva waliovunja sheria za Usalama Barabarani katika eneo
la shule yao.
Pia Kamanda Mutafungwa alilipongeza Shirika la Amend kwa kujitoa
kwao na kazi kubwa wanayoifanya ya kuhakikisha wanatumia Mahakama hiyo
ya watoto kutoa elimu kwa madereva nchini nzima hususani kwenye maeneo ya shuleni.
"Niwapongeze sana Amend wanafanya kazi kubwa sana
katika kuhakikisha wanatoa elimu hii kupitia watoto hawa na sisi
tutaendelea kutoa kila ya aina ya ushirikiano kwao, nakuyataka Mashirika
mengine kujitokeza ili kuhakikisha ajali za barabarani
zinamalizika,"amesema.
Akizungumzia kuhusu ajali za barabrani
amesema kuwa, kwa asilimia kuwa ajali zimepungua sana na wataendelea
kutoa elimu ya usalama barabarani ili kuona mwisho wa siku ajali
zinamalizwa kwa asilimia kubwa kama si kutokomezwa kabisa.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Wilbroad Mutafungwa
akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa Mahakama ya
Watoto iliyokuwa ikiendshwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Olimpio
mkoani Dar es Salaam iliyokuwa na lengo la kutoa elimu ya Usalama
Barabarani kwa wananchi ambapo ametumia nafasi hiyo kuelezea hatua
mbalimbali ambazo zinachukuliwa na jeshi hilo kifikisha elimu hiyo kwa
wananchi. (DIRAMAKINI).
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Amend, Simon
Kalolo amesema kuwa wao kama wadau wa usalama barabarani
kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani kazi
kubwa wanayofanya nikutoa elimu ya usalama barabarani.
Amesema
kuwa, katika kuhakikisha wanapunguza ajali hizo za usalama wa barabarani
hivi sasa wamekuja na Mahakama ya Watoto Shuleni ambayo kazi yake
kubwa itakuwa ni kuwahukumu madereva ambao wanavunja sheria za alama za
usalama barabarani na kusababisha ajali zisizo za lazima.
Amefafanua
kuwa, wamekuja na Mahakama hiyo ikiwa ni sehemu ya ubunifu kwa lengo la
kufikisha meseji ya moja kwa moja kwa watumiaji wa vyombo vya moto ,
kwani anaamini watumiaji wengi wanapohojiwa na watoto wadogo kwa makosa
ambayo wanayafanya watajisikia vibaya na ni rahisi kubadilika.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Wilbroad Mutafungwa
(kulia) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Shirika la Amend Tanzania,
Simon Kalolo (katikati) na Meneja Programu wa Shirika hilo, Neema Swai
(kushoto) baada ya kumalizika kwa Mahakama ya Watoto iliyokuwa
inasikiliza kesi ya madereva waliovunja sheria za Usalama
Barabarani.Mahakama hiyo imeendeshwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi
Olimpio mkoani Dar es Salaam.
Wanafunzi
wa Shule ya Msingi Olimpio mkoani Dar es Salaam ambao wapo kwenye
Programu ya Makakama ya Watoto wakiwa makini kuangalia mmoja wa madereva
akiandika kiapo cha kutorudia kuvunja Sheria ya Usalama Barabarani
baada ya kukiri mbele ya Wanafunzi hao kuvunja sheria hizo baada ya
kutosimama kwenye kivuko cha waenda kwa miguu kilichopo nje ya shule
hiyo .Wa kwanza kushoto ni Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama
Barabarani Wilbroad Mutafungwa akifuatilia uendeshaji kesi uliokuwa
unafanywa na wanafunzi hao wakati Makakama ya Watoto ikiendelea.
Mmoja
ya madereva walikamatwa kwa kosa la kuvunja sheria ya Usalama
Barabarani akisoma kiapo cha kutorudia tena kuvunja sheria hizo mbele ya
Wanafunzi waliokuwa wanaoendesha Mahakama ya Watoto katika Shule ya
Msingi Olimpio mkoani Dar es Salaam.Wa kwanza kushoto aliyekaa kwa
wanafunzi hao ni Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama
Barabarani Wilbroad Mutafungwa akisikiliza mwenendo wa kesi katika
mahakama hiyo.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi ,Kikosi cha Usalama Barabarani, Wilbroad Mutafungwa (
wa kwanza kushoto waliokaa) akiwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi
Olimpio jijini Dar es Salaam wakati wanafunzi hao wakisikiliza kesi za
madereva waliovunja sheria za Usalama Barabarani kupitia programu ya
Makakama ya Watoto yenye lengo la kutoa elimu ya usalama
barabarani.Aliyekaa mbele ya Kamanda Mutafungwa na wanafunzi hao ni
mmoja wa madereva ambaye alikamatwa na askari wa Usalama Barabarani kwa
kosa la kutosimama kwenye kivuko cha waenda kwa miguu kilichopo eneo la
shule hiyo.
"Huu
ni ubunifu tu ambao sisi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo
cha usalama barabarani tumeufanya na kwakweli Mahakama hiii imekuwa
ikifanya vizuri sana na hadi sasa tumeshazifkkia shule karibu nane na
lengo nikuona tunatekeleza mradi huu kwa nchi nzima,"amesema Kalolo.
Ameongeza
kuwa, watoto hao wamekuwa wabunifu na wengi wao ukiwauliza wanasema
wanatamani waje kuwa Mahakimu na hiyo inatokana na uhodari na ujasiri
wanaouonyesha katika kuuliza maswali kwa madereva ambao wanafanya makosa
hayo.
Nao
watoto hao kwa pamoja wamesema, madereva wanatakiwa wawe makini na
wasiwachukulie poa kwa sababu wao ni watoto wadogo kwani wakifanya
makosa na kufikishwa mbele ya Mahakama yao wajue watakabiliana na
maswali magumu na watapata hukumu na kula kiapo cha ahadi cha kutofanya
tena makosa ambayo yanapelekea kusababisha ajali hususani kwa watembea
kwa miguu (vivuko)
No comments:
Post a Comment