NAIBU
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo
Mathew ameutaka uongozi wa Kata ya Katoro mkoani Geita kwenda kuzingatia
sifa na vigezo kwa ajira zitakazotolewa ili kukamilisha zoezi la Anuani
za Makazi.
Naibu
Waziri Kundo ameyasema hayo katika Kata ya Katoro iliyopo Wilaya ya
Geita Vijijini mkoani Geita wakati wa kikao kazi cha viongozi na
watendaji wa kata hiyo kuhusu utekelezaji wa operesheni Anuani za
Makazi.
Naibu
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi
Kundo Mathew (Mb) akizungumza wakati wa kikao kazi cha kuwajengea uelewa
viongozi na watendaji kuhusu utekelezaji wa operesheni ya Anuani za
Makazi kilichofanyika katika Kata ya Katoro iliyopo Wilaya ya Geita
Vijijini mkoani Geita.
“Sitegemei
kuona kwamba vijana ambao wanakwenda kupata ajira katika zoezi hili
wanatoka Dar es Salaam, wanatoka Mwanza wala wanatoka Geita, natarajia
kuona kwamba zoezi hili linakwenda kusimamiwa na wazawa na ajira hizi
ziende zikanufaishe wananchi wa kata ambayo zoezi linafanyika,”amesema
Mhandisi Kundo.
Aidha,
Mhandisi Kundo amewaeleza kuwa pamoja na faida nyingine, mfumo huo
utaiwezesha Serikali ya Mhe.Rais Samia kuleta maendeleo katika Kata ya
Katoro kwa urahisi kwani idadi ya watu wanaoishi katika kata hiyo
itakuwa inajulikana baada ya kushiriki kikamilifu katika maozezi hayo
mawili ya anwani za makazi na lile la Sensa ya Watu na Makazi.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Huduma za Posta wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na
Teknolojia ya Habari, Caroline Kanuti (wa kwanza kushoto) akitoa
maelekezo jinsi ya kupata Postikodi ya Kata kwa kutumia simu ya mkononi
wakati wa kikao kazi cha kuwajengea uelewa Viongozi na Watendaji wa Kata
ya Katoro iliyopo Wilaya ya Geita Vijijini mkoani Geita kuhusu
utekelezaji wa operesheni Anuani za Makazi
Mkuu
wa Wilaya ya Geita, Mhe. Wilson Shimo akizungumza wakati wa kikao kazi
cha kuwajengea uelewa Viongozi na Watendaji wa Kata ya Katoro kuhusu
utekelezaji wa operesheni Anuani za Makazi. Kikao kazi hicho
kilifunguliwa na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya
Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew (Mb).
Meneja
wa TCRA Kanda ya Ziwa, Mhandisi Francis Mihayo akizungumza na viongozi
na watendaji wa Kata ya Katoro iliyopo Wilaya ya Geita Vijijini mkoani
Geita kuhusu utekelezaji wa operesheni Anuani za Makazi. Kikao kazi
hicho kilifunguliwa na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia
ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew(Mb).
Mkurugenzi
Msaidizi wa Huduma za Posta wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na
Teknolojia ya Habari, Caroline Kanuti akizungumza wakati wa kikao kazi
cha kuwajengea uelewa Viongozi na Watendaji wa kata ya Katoro iliyopo
Wilaya ya Geita Vijijini Mkoani Geita kuhusu utekelezaji wa operesheni
Anwani za Makazi. Kikao kazi hicho kilifunguliwa na Naibu Waziri wa
Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew
(Mb).
Awali
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo amesema wananchi wake tayari
wanalifahamu vizuri jambo la anuani za makazi na ni matumaini yake
kwamba kazi nzuri itakwenda kufanywa na wakazi hao wa Kata ya Katoro ili
kuhakikisha na wao wanajumuishwa kikamilifu katika maendeleo
yatakayoletwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.
Zoezi
la utekelezaji mfumo wa Anuani za Makazi linatakiwa kukamilika mapema
ifikapo mwezi Mei, 2022 ili kuwezesha zoezi lingine la Sensa ya Watu na
Makazi likafanyike kwa urahisi mwezi Agosti, 2022.
No comments:
Post a Comment