Mwenyekiti
wa Kudumu wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Naghenjwa
Kaboyoka akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo katika kikao cha kupokea
taarifa ya utekeleza wa mradi wa Backbone Transmission Investment
Project (BTIP) wakati kamati hiyo ilipokuwa katika ziara ya ukaguzi wa
mradi huo mkoaniSingida jana.
Mratibu wa mradi huo Mhandisi Emmanuel Manirabona akiwaelekeza jambo wajumbe wa kamati hiyo wakati wa ukaguzi wa mradi huo.
Wajumbe wa kamati hiyo wakipokea taarifa hiyo.
Mkaguzi
Mkuu wa Nje kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG), Priscus Ngowi akitoa taarifa ya ukaguzi wa mradi huo.
Mjumbe wa kamati hiyo Mhandisi Isack Kamwele akichangia jambo katika kikao hicho cha kupokea taarifa ya mradi huo.
Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Japhet Hasunga akizungumza kwenye kikao hicho.
Wafanyakazi wa TANESCO wakiwa kwenye kikao hicho.
Muonekano wa mradi huo.
Safari ya kuelekea kukagua mradi huo ikiendelea.
Meneja
wa Usimamizi wa Vifaa vya Umeme wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
Mhandisi Timoth Mgaya akiwaelekeza wajumbe wa kamati hiyo kuhusu mradi
huo.
Mjumbe
wa Bodi ya TANESCO Mhandisi Abdallah Hashim akitoa maelezo kwa wajumbe
wa kamati hiyo. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Japhet
Hasunga na kulia ni Mwenyekiti wa Kudumu wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za
Serikali (PAC), Naghenjw Kaboyoka.
Ukaguzi wa mradi huo ukiendelea.
Ulinzi ukiwa umeimalishwa wakati wajumbe wa kamati hiyo walipokuwa katika ziara ya kukagua mradi huo.
Na Dotto Mwaibale, Singida | KAMATI
ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imelipongeza Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO) na kuridhishwa kwa kutekeleza vizuri mradi wa
Backbone Transmission Investment Project (BTIP) awamu ya pili
unaofanywa katika mikoa ya Iringa, Dodoma, Shinyanga na Singida.
Pongezi
hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge wa kamati hiyo
Naghenjwa Kaboyoka wakati kamati hiyo ilipotembelea kukagua mradi huo
mkoani Singida jana.
“Tumefika
leo kutembelea mradi huu wa kimkakati ambao serikali imetumia fedha
nyingi kwa kufadhiliwa kwa fedha za mkopo kutoka kwa wahisani wa
maendeleo ya sekta ya Nishati na kuridhishwa na utekelezaji wake” alisema Kaboyoka.
Kaboyoka
alisema changamoto walizoambiwa na watekelezaji wa mradi huo
wamezichukua na watazifanyia kazi kwa kuziwasilisha kunakohusika.
Mratibu
wa mradi huo Mhandisi Emmanuel Manirabona akitoa taarifa mbele ya
kamati hiyo alisema Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango na
wahisani wa maendeleo wa sekta ya Nishati walikubaliana kutumia akiba
iliyopatikana kwa awamu ya isaidie kutekeleza awamu ya pili ya mradi.
“Awamu
hii ya pili inafadhiliwa kwa fedha za mkopo kutoka kwa wahisani wa
maendeleo ya sekta ya Nishati ambao ni Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB) ,Shirika la Kimataifa la Kimataifa la Japan (JICA) pamoja na
Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) kwa jumla ya kiasi cha Dola za
Marekani 120 Milioni” alisema Manirabona.
Alisema
katika kuhakikisha kuwa mradi huo unatekelezwa kulingana na mahitaji
yaliyotolewa kwa wakandarasi kwa ubora unaotakiwa na kuhakikisha kuwa
TANESCO inapata mradi wenye thamani ya fedha itakazotoa ilifanya
manunuzi ya Mkandarasi Mshauri kusimamia mradi huo kwa niaba ya uongozi
wa shirika.
Mhandisi
Manirabona aliongeza kuwa shirika hilo limeweka timu ya mradi
inayoundwa na Mratibu, mameneja wa miradi na wahandisi wa mradi
watakaosimamia kila siku shughuli za mradi.
Alisema
faida za mradi huo kwa nchi yetu mara utakapokamilika utaongeza uwezo
wa kusafirisha umeme kwa wingi kwenda kwenye mikoa yenye mahitaji
makubwa ya umeme, kuunganishwa kwa gridi ya taifa kwenye kanda ya Afrika
Mashariki (EAPP) kupitia mradi wa Kenya, Tanzania na Kusini (SAPP)
kupitia mradi wa Tanzania, Zambia na kuweza kufanya biashara ya kuuziana
nishati ya umeme hivyo kukuza uchumi na pato la taifa kwa ujumla.
Alitaja
faida nyingine kuwa ni kupunguza upotevu wa umeme na kulisaidia Shirika
kukwepa gharama nyingi zinazotokana na upotevu huo.
Mkaguzi
Mkuu wa Nje kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG), Priscus Ngowi alitaja baadhi ya changamoto walizoziona
baada ya matokeo ya ukaguzi ya mwaka wa fedha ulioishia Juni 2021 ya
utekelezaji wa mradi huo kuwa ni Mabadiliko ya sheria za kodi kwa
miradi ambayo imekwishaanza kutekelezwa, Mabadiliko ya viwango vya
malipo kwa Wakala wa Barabara (TANRODS) kwa kuzidisha uzito wa mizigo,
Ucheleweshaji wa malipo kwa mkandarasi kwa miradi inayopokea malipo moja
kwa moja kutoka kwa mfadhili na kushindwa kukamilika kwa vituo vya
Iringa na Shinyanga.
No comments:
Post a Comment