Wafugaji Jamii ya Wamasai wakiwa kwenye mkutano wa kujadili htima yao wilayani Ngorongoro mkoani Arusha jana.
Na Mwandishi Wetu, Arusha |
WAFUGAJI wa jamii ya wamasai wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wamesema
kamwe hawajawahi na hawatafanya hivyo kuwazuia watu wanaoishi eneo la
Ngorongoro wanaotaka kuhama kwa hiari yao wenyewe kwani wanaofanya hivyo
ni uhuru wao.
Aidha,
wamesema serikali nayo kwa upande wao isimlazimishe mtu yeyote kuondoka
eneo la Ngorongoro hasa kutokana na baadhi ya watu wakiwamo wabunge
kutaka majeshi yatumike kuwaondoa.
Walisema
hayo juzi (Machi 13) katika mkutano wa wafugaji wa tarafa ya Ngorongoro
uliofanyika jijini Arusha kujadili hatma yao kuhusiana na mgogoro
unaoendelea ambapo serikali inataka wafugaji wanaoishi ndani ya eneo la
hifadhi ya Ngorongoro kuondoka ili kupisha uhifadhi.
Joseph
Ole Shangay akizungumza wakati wa mkutano huo alisema serikali isiweke
mazingira yeyote ya kumlazimisha mtu aondoke bila ridhaa yake kwani
kufanya hivyo itakuwa ni kukiuka haki za binadamu.
"Baadhi
ya watu wanasema waondoke sababu ni maskini, kama kweli kumuondoa mtu
eneo kwasbabu tu ni maskini basi hii nchi tuhame maana inaogelea kwenye
umaskini," alisema.
Ole
Shangay ambaye pia ni wakili alisema kinachofanywa na serikali ni sawa
na fisi akitaka kuwala watoto wake anawayengeneza wawe na halufu kama ya
mbuzi ili apate sababu ya kuwaua na kuwala
Kuhusu
idadi ya mifugo, alisema kwamujibu wa ripoti iliyofanyika 2017
ilionesha kuwa Ngorongoro kuna mifugo 230,000 ambayo ni sawa na ongezeko
la takribani mifugo 20,000 toka mwaka 1959 ambalo ni ongezeko dogo
sana.
Oleshangay
alisema kimsingi wafugaji halisi wa eneo la Ngorongoro hawana mpango wa
kuhama eneo hilo na kuiomba serikali isitishe mchakato wake wa kutaka
kuwaondoa kwababu wapo Ngorongoro kisheria na sio kama wavamizi.
Aidha,
alisema jamii ya wamasai hawana mahusiano yeyote ya kiimani wala ya
kihistoria na eneo linaloitwa Malya ambako hivi karibuni kulifanyila
mkutano na viongozi wa serikali kuhudhuria.
Mwenyekiti
wa Baraza la Wafugaji Ngorongoro, Edward Maura, alisema inashangaza
kuona serikali inakazana na mipango ya kutaka kuwaondoa wenyeji wa
Ngorongoro kwa madai kuwa hidadhi ya Ngorongoro ipo hatarini kupotea
kitua ambacho hakina ukweli.
"Watanzania
na dunia nzima puuzeni taarifa ya kwamba watu wa Ngorongoro wamekubali
kuhama kwa hiari yao, puuzeni hiyo sio habari, hatuna mpango wala
mkakati wa kukubaliana na mtu yeyote kuondoka eneo la Ngorongoro," alisema.
Maura
alisema Ngorongoro ina mfumo rasmi wa uongozi wakiwamo malaigwanan,
wenyeviti wa vijivini, madiwani na mbunge hawakuhudhuria mkutano wa hivi
karibuni ulioitishwa na Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa, uliofanyika
jijini Arusha.
Alisema
hifadhi ya Ngorongoro imekuwa ikipata sifa kimataifa na kuongezeka kwa
mapato kila mwaka hivyo sababu ya kwamba hifadhi ipo hataririni kupotea
kutokana na watu na mifugo wanaoishi ndani haina msingi propaganda hiyo
inafanywa kwa maslahi ya watu wachache wenye maslahi yao binafsi.
Kwa
upande wake kiongozi wa Malaigwanani Ngorongoro, Metui OleShaudo,
alisema inasikitisha baadhi ya viongozi kuwaita wananchi wa Ngorongoro
kwamba ni raia wa Sudani na kwamba sio raia wa Tanzania wakati sio kweli
wao ni Watanzania halali wa kuzaliwa.
"Endapo sisi ni wasudani basi tusipelekwe Handeni aje rais wa Sudani tuzungumze naye hapa na tuhamishiwe twende Sudan," alisema.
Oleshaudo
alisema wako tayari kukaa na serikali kuzungumza namna ya kuendeleza
uhifadhi katika hifadhi ya Ngorongoro lakini sio suala la kuhama eneo la
Ngorongoro.
Naye
Lazaro Saitoti alisema inashangaza kuona mikakati ikiendelea kupangwa
kutaka kuwaondoa eneo la Ngorongoro wakati kimsingi hakuna ushahidi
wowote unaonyesha kuwa wafugaji wanaoishi eneo hilo wanahatarisha maisha
ya wanyamapori.
"Tunahitaji
serikali ije na 'fact' je kwa muda wote ambao tumekuwa Ngorongoro toka
tulipotoka Serengeti ni ngo'mbe gani amekula Simba, ni mbuzi gani
amekula chui au pundamilia maana ndo mifugo ambao tunaishi nao kwa muda
wote na hakuna mnyamapori aliyeuawawa na mifugo yetu," alisema.
Diwani
wa Kata ya Endulen,James Moringe, amemuomba rais Samia Suluhu Hassan
kuruhusu miradi ya maendeleo iliyosimamishwa tarafa ya Ngorongoro
iendelee kujengwa kwasababu kuisimamisha kunawathiri wananchi.
Moringe
alisema katika kikao walichofanya na Waziri Mkuu Februari 17, mwaka huu
wafugaji walieleza hujuma mbalimbali dhidi ya wanyamapori zinazofanyika
ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) lakini hakuna hatua
zozote zilizochukuliwa kwa wahusika ambao ni watumishi ndani ya hifadhi
hiyo.
No comments:
Post a Comment