A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, March 12, 2022

OFISI YA RAIS TAMISEMI YAVITAKA VYUO VYA ELIMU YA UFUNDI KUTENGENEZA MFUMO RAFIKI WA UTOAJI TAARIFA.

 Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI imeviagiza vyuo vyote vya elimu ya ufundi nchini kutengeneza mfumo utakaomuwezesha kila mtu kupata taarifa mhimu za udahili wa wananfunzi wanaochaguliwa na ofisi hiyo kujiunga na taasisi mbalimbali za elimu.

Agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi wa elimu ya Sekondari TAMISEMI Bi. Hadija Mcheka kwenye mkutano wa kujadili mafanikio na changamoto za udahili wa wananfunzi waliochaguliwa na TAMISEMI kujiunga na vyuo vya elimu na mafunzo ya ufundi hapa nchini.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi.Mcheka amesema kunachangamoto ya wananfunzi wanaochaguliwa kujinga na vyuo vya elimu ya fundi hapa nchini kushindwa kuthibitisha kwa wakati watajiunga na vyuo hivyo kwa sababu ya kutokupata taarifa kwa wakati hasa wale waishio vijijini hali inayochangia kuwa na malalamiko mengi ya wanafunzi kuuzwa kwa wanfasi zao.

Amesema kutokana na changamoto hiyo TAMISEMI imewataka wakuu wa vyuo kusimamia udahili wa wanafunzi wote wanajiunga katika vyuo vyao na kutafuta mbinu Rafiki ya kutoa taarifa ambayo itawafikia wanafunzi wote pamoja na wavijijini ambao wengi wamekuwa kukikosa taarifa kwa wakati.

Kwa upande wake Dokta Jofrey Oleka Mkurugenzi ithibiti na ufuatiliaji tathimin NACTEVAT amewataka wakuu vyuo udahili wa wanfunzi kwa kufuata misingi na muungozo wa NACTEVAT kwa kuchua wanafunzi kutokana na uwezo wa chou.

Aidha Serikali imelidhia ombi la wakuu wa vyuo la kufunguliwa kwa udahiri wa mwezi watatu kwa wanafunzi wanajiunga na vyuo vya elimu ya ufundi isipokuwa kwa wale wanaotaka kujiunga katika vyuo vya Afya mpaka pale serikali itakapotoa tamko linguine.




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages