Afisa
Mikopo Mwandamizi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
(HESLB), Sophia Saidan akitoa huduma kwa wateja mbalimbali waliotembelea
Banda la HESLB Jumapili (Machi 13, 2022) Mkoani Tanga wakati wa kampeni
ya SIFURISHA inayoendelea katika Ofisi za Halmashauri ya Jiji la Tanga.
Kampeni hiyo inalenga kuhumasisha urejeshaji wa mikopo ya elimu ya juu
kutoka kwa wanufaika.
Maafisa
Mikopo wa HESLB wakitoa huduma mbalimbali kwa wateja Jumapili Machi 13,
2022 Mkoani Tanga wakati wa Kampeni ya SIFURISHA inayolenga kuhamasisha
urejeshaji wa mikopo ya elimu ya juu inayoendelea katika Ofisi za
Halmashauri ya Jiji la Tanga.
Meneja
wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Ofisi ya Arusha,
PatricK Shoo akimkabidhi barua ya kumaliza deni la Mkopo wa elimu ya
juu TZS 11,345,845.20/- Jumapili (Machi 13, 2022) Mkoani Tanga, Hakimu
wa Mahakama ya Mwanzo Wilaya ya Handeni, Mhe. Yusuph Abdallah wakati wa
kampeni ya SIFURISHA inayoendelea katika Ofisi ya Halmashauri ya Jiji la
Tanga.
Afisa
Mikopo Mwandamizi wa HESLB, Sunday Charles akimkabidhi barua ya
kumaliza deni la mkopo wa elimu ya juu, TZS 9,736,900.90, mtumishi wa
Halmashauri ya Jiji la Tanga Mary Siphaelly Jumapili (Machi 13, 2022)
mara ya baada kulipa kiasi cha TZS 1,888,000/- na kumaliza deni la mkopo
huo wakati wa kampeni ya SIFURISHA inayoendelea katika Ofisi za
Halmashauri ya Jiji la Tanga. (PICHA NA HESLB)
No comments:
Post a Comment