Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akioongozwa
na Mkuu wa wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza Bi. Senye Ngaga alipowasili
kwa ajili ya kuzindua Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Sengerema
mkoani Mwanza tarehe 21 Machi 2022.
Mkuu
wa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza Senye Ngaga akizungumza wakati wa
uzinduzi wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Sengerema mkoani
Mwanza tarehe 21 Machi 2022. Kushoto ni mwenyekiti wa Halmashauri ya
Sengerema Yanga Mayanga na wa pili kushoto ni Msajili wa Mabaraza nchini
Stella Tullo
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza
na uongozi pamoja na watendaji wa sekta ya ardhi wilayani ya Sengerema
mkoani Mwanza kabla ya kuzindua Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya
tarehe 21 Machi 2022.
===== ==== =====
Na Munir Shemweta, WANMM SENGEREMA
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewaonya
wananchi wanaojenga au kupanda mazao kwenye maeneo yanayopangwa
kutwaliwa na Serikali kwa shughuli mbalimbali zikiwezo za uwekezaji
maarufu kama ‘’Tegesha’ mara baada ya kutangazwa tarehe ya ukomo ya
kufanya maendelezo.
Dkt
Mabula alitoa onyo hilo leo tarehe 21 Machi 2022 wilayani Sengerema
mkoani Mwanza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya
ya Sengerma.
Alisema,
kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wananchi kununua maeneo yaliyopangwa
kutwaliwa na serikali kwa ajili ya shughuli mbalimbali na kuanza kufanya
maendelezo ya kujenga ama kupanda mazao ili kupata fidia wakati wa
zoezi la uthamini huku maeneo hayo yakiwa yametangazwa tarehe ya ukomo
ya kufanya maendelezo.
Kwa
mujibu wa Dkt Mabula, Serikali ya Awamu ya Sita haitavumulia tabia hiyo
kwa kuwa jambo hilo linaiingizia hasara serikali na kusisitiza kuwa,
wananchi watakaobainika kufanya vitendo vya Tegesha basi watachukuliwa
hatua kali ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
‘’Mtu
anapanda Mualovela mlimani na inaonekana mualovela wenyewe umechomekwa,
nisisitize kuwa, kama kuna kitu kilichoongezeka baada ya kuchukuliwa
picha ya anga na kutangazwa kwa tarehe ya ukomo ya maendelezo basi
hakitalipwa na serikali italipa kile kinachoonekana kwenye picha ya
anga’’ alisema Dkt Mabula.
Dkt
Mabula alitolea mfano wa eneo la Mlima Nyanzaga uliopo wilayani
Sengerema mkoani Mwanza kuwa, kuna baadhi ya wananchi wamenunua eneo la
mlima na kuanza kusafirisha migomba nyakati za usiku ili kutegesha kwa
lengo la kupata fidia mara tu baada ya kusikia serikali inataka kulitwaa
eneo hilo.
Alisema,
hali hiyo haiwezi kuvumiliwa hata kidogo na serikali italipa fedha kwa
yale maeneo yaliyoonekana katika picha za anga ambazo Wizara ya Ardhi
ilizichukua mapema kwa lengo la kuondoa mgongano wakati wa kulipa fidia.
Akigeukia
uzinduzi wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Sengerema, Dkt
Mabula amesema uzinduzi wa baraza hilo umelenga kusogeza huduma kwa
wananchi wa wilaya hiyo ya Sengerema ambao awali walikuwa wakiifuata
wialayni Geita.
Aliwataka
Wakuu wa wilaya na Wakurugenzi kwenye wilaya ambazo Mabaraza ya Ardhi
na Nyumba ya Wilaya hayajaanza kutoa huduma, kutoa kipaumbele kwa
shughuli za mabaraza kwa kutenga maeneo ya ofisi kuwezesha mabaraza
kuanza kutoa huduma ili kuwaondolea wananchi usumbufu wa kwenda kupata
huduma katika wilaya nyingine.
No comments:
Post a Comment