Meneja
Mradi wa Usafi wa Mazingira Mjini wa Shirika la SNV,Bw. Olivier Germain
akielezea kuhusu ujenzi wa Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa
Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa
Shinyanga.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa
wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amefungua Choo cha Kisasa cha
umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha
Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la
Uholanzi (SNV – Netherlands Development Organization) na Halmashauri ya
Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG) na
kufadhiliwa na Serikali ya Uholanzi.
Uzinduzi wa Choo cha
Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika
Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga (Ibinzamata) umefanyika leo Jumatano
Machi 23,2022 na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa afya na mazingira
wakiongozwa na Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi
kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.
Meneja
Mradi wa Usafi wa Mazingira Mjini wa Shirika la Maendeleo la Uholanzi,
Bw. Olivier Germain amesema ujenzi wa Choo cha Kisasa cha umma pamoja na
Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa
Shinyanga ulioanza Mwezi Oktoba 2021 na kumalizika Mwezi Machi 2022
umetumia zaidi ya shilingi Milioni 160.
Ameyataja
maeneo muhimu ya mradi huo kuwa ni vyumba vya choo kwa ajili ya wanaume
na wanawake ambavyo pia vina sehemu kwa ajili ya watu wenye mahitaji
maalumu (Kama vile walemavu, wajawazito, wagonjwa, watoto, wazee nk)
Mabafu ya kuogea na vyumba vya kubadilishia nguo, sehemu za haja ndogo
kwa wanaume (Urinals), Mashine maalumu ya kuuzia taulo za kike
(Pads-Vending Mashine) zitakazouzwa kwa shilingi 200/= katika eneo la
vyumba vya wanawake.
Germain amezitaja sehemu zingine kuwa ni
Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant), Maduka na mgahawa pamoja na
mfumo wa kuvuna maji ya mvua.
Germain amewasihi watumiaji wa
choo hicho cha kisasa kuzingatia suala la usafi, ulinzi wa kila mmoja wa
miundombinu ya choo, pamoja na kutumia choo hicho kwa ajili ya kupata
gesi asilia.
“Naomba mtumie na kutunza mradi huu ili uwe
endelevu, tumieni ili tupate pia gesi asilia. Choo hiki ni kwa ajili ya
kila mtu kwani tumejenga kulingana na mahitaji ya watu wote wakiwemo
wenye ulemavu, watoto na wazee lakini kuna chumba cha kujistiri kwa
akina mama na taulo za kike ‘pedi’ zinapatikana ndani ya choo hiki bora
na nafikiri hakuna choo cha namna hii hapa Tanzania”,amesema Germain.
Akizindua
mradi huo kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta
Mboneko, Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi
amelishukuru Shirika la SNV kwa kushirikiana na Manispaa ya Shinyanga na
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) kwa
kujenga choo hicho cha kisasa na Mtambo wa Gesi asilia na kwamba mradi
huo utakuwa shamba darasa na utatumika kuiingizia mapato halmashauri ya
Manispaa ya Shinyanga.
“Naomba tuutunze mradi huu ili uwe
endelevu. Mradi huu ni shamba darasa na tutautumia kujifunza mambo mengi
ikiwemo masuala ya usafi na matumizi ya gesi asilia. Lakini pia ndani
ya Jengo hili kuna vyumba vya biashara na mgahawa ambavyo vyote
vitachangia katika kuiingizia mapato Manispaa ya Shinyanga”,amesema
Chambi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mhe.
Jomaary Satura ameahidi kutunza mradi huo na kuwataka wadau wanaofanya
shughuli zao katika Kituo cha mabasi kushirikiana kutunza mradi huo.
“Tuwashukuru
wenzetu SNV kwa mradi huu na mradi mingine wanayotekeleza katika
Manispaa yetu. Sisi dhamira yetu ni kuona Manispaa ya Shinyanga inakuwa
kinara wa utunzaji mazingira nchini. Choo hiki kitakuwa kielelezo cha
ustaarabu wetu na tayari tumefunga taa katika Stendi hii hivyo wananchi
wataweza kufanya shughuli zao usiku na mchana”,amesema Satura.
Naye
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko na
Diwani wa Viti Maalumu Mhe. Shella Mshandete wameipongeza SNV kujenga
choo bora na cha kisasa kinachozingatia mahitaji ya watu wote wakiwemo
wenye ulemavu, watoto na wanawake.
Muonekano
wa sehemu ya mbele ya Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi
asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga
vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri
ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG)
na kufadhiliwa na Serikali ya Uholanzi. Picha na Kadama Malunde -
Malunde 1 blog
Katibu
Tawala Wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi kwa niaba ya Mkuu wa
wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) akizindua Choo cha
Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika
Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na Shirika la
Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga. Wa
pili kushoto ni Meneja Mradi wa Usafi wa Mazingira Mjini wa Shirika la
SNV,Bw. Olivier Germain.
Katibu
Tawala Wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi (katikati kulia)
akisoma maandishi baada ya kuzindua Choo cha Kisasa cha umma pamoja na
Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa
Shinyanga vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga. Anayepiga makofi kushoto ni Meneja
Mradi wa Usafi wa Mazingira Mjini wa Shirika la SNV,Bw. Olivier
Germain.
Maandishi
katika Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio –
Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na
Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya
Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG) na kufadhiliwa
na Serikali ya Uholanzi.
Wananchi
wakifuatilia uzinduzi wa Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa
Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga
vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri
ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG)
na kufadhiliwa na Serikali ya Uholanzi.
Katibu
Tawala Wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi kwa niaba ya Mkuu wa
wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) akikata utepe wakati
akizindua Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio
– Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na
Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya
Shinyanga.
Meneja
Mradi wa Usafi wa Mazingira Mjini wa Shirika la SNV,Bw. Olivier Germain
akielezea kuhusu ujenzi wa Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa
Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa
Shinyanga.
Mhandisi
wa Shirika la SNV, Hezron Magambo akielezea kuhusu ujenzi wa Choo cha
Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika
Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga.
Muonekano
wa sehemu ya Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia
(Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga
vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri
ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG).

wa sehemu ya maduka katika Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa
Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga
vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri
ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG).
Afisa
Afya Manispaa ya Shinyanga Sanya Anthony (aliyeshikilia kipaza sauti
katikati) akielezea kuhusu ujenzi wa Choo cha Kisasa cha umma pamoja na
Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa
Shinyanga vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira
(WASH SDG).
Afisa
Afya Manispaa ya Shinyanga Sanya Anthony (kulia) akielezea mfumo wa
Gesi asilia katika Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi
asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga
vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri
ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG).
Katibu
Tawala Wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi (kushoto) akinawa
mikono baada ya kuingia ndani ya Choo cha Kisasa cha umma katika Kituo
cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga kilichojengwa na Shirika la Maendeleo la
Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa
Usafi wa Mazingira (WASH SDG). Kulia ni Meneja Mradi wa Usafi wa
Mazingira Mjini wa Shirika la SNV,Bw. Olivier Germain.
Katibu
Tawala Wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi akiangalia choo kwa
ajili ya watu wenye mahitaji maalumu ndani ya Choo cha Kisasa cha umma
katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga kilichojengwa na Shirika la
Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG). Kulia ni Meneja Mradi wa
Usafi wa Mazingira Mjini wa Shirika la SNV,Bw. Olivier Germain.
Afisa
Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga Angel Mwaipopo akimwelezea
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi kuhusu Mashine
ya kununulia Taulo za kike kwa shilingi 200/= tu katika eneo la vyumba
kwa ajili ya wanawake ndani ya Choo cha Kisasa cha umma katika Kituo cha
Mabasi Mkoa wa Shinyanga kilichojengwa na Shirika la Maendeleo la
Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa
Usafi wa Mazingira (WASH SDG).
Wadau
wakiwa katika eneo la kununulia Taulo za kike kwa shilingi 200/= tu
katika eneo la vyumba kwa ajili ya wanawake ndani ya Choo cha Kisasa cha
umma katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga.
Katibu
Tawala Wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi (wa tatu kushoto)
akizungumza jambo katika sehemu ya haja kwa wanaume ndani ya Choo cha
Kisasa cha umma katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga kilichojengwa
na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya
Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG).
Moja
ya vyumba katika Choo cha Kisasa cha umma katika Kituo cha Mabasi Mkoa
wa Shinyanga kilichojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira
(WASH SDG).
Sehemu
ya kunawia mikono eneo la wanaume katika Choo cha Kisasa cha umma
katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga kilichojengwa na Shirika la
Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG).
Eneo
la wanawake ndani ya Choo cha Kisasa cha umma katika Kituo cha Mabasi
Mkoa wa Shinyanga kilichojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi
(SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa
Mazingira (WASH SDG).

Mkurugenzi
wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaary Satura akizungumza wakati wa
uzinduzi wa Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia
(Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga
vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri
ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG)
na kufadhiliwa na Serikali ya Uholanzi.
Diwani
wa Viti Maalumu Mhe. Shella Mshandete akizungumza wakati wa uzinduzi wa
Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas
Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na
Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya
Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG) na kufadhiliwa
na Serikali ya Uholanzi.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko akizungumza wakati
wa uzinduzi wa Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia
(Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga
vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri
ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG)
na kufadhiliwa na Serikali ya Uholanzi.
Katibu
Tawala Wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi akizungumza kwa niaba
ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko wakati wa uzinduzi
wa Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas
Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na
Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya
Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG) na kufadhiliwa
na Serikali ya Uholanzi.
Katibu
Tawala Wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi akipanda mti kwa niaba
ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko wakati wa uzinduzi
wa Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas
Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na
Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya
Shinyanga kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG) na kufadhiliwa
na Serikali ya Uholanzi.
Katibu
Tawala Wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi akipiga picha ya
kumbukumbu na viongozi wa Shirika la SNV, Manispaa ya Shinyanga na wadau
wa afya na mazingira baada ya uzinduzi wa Choo cha Kisasa cha umma
pamoja na Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha
Mabasi Mkoa wa Shinyanga vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la
Uholanzi (SNV) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Katibu
Tawala Wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi akipiga picha ya
kumbukumbu na Viongozi mbalimbali na wanafunzi wa shule ya msingi
Ibinzamata baada ya uzinduzi wa Choo cha Kisasa cha umma pamoja na
Mtambo wa Gesi asilia (Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa
Shinyanga vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Katibu
Tawala Wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi akipiga picha ya
kumbukumbu na wadau katika kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga baada ya
uzinduzi wa Choo cha Kisasa cha umma pamoja na Mtambo wa Gesi asilia
(Bio – Gas Plant) katika Kituo cha Mabasi Mkoa wa Shinyanga
vilivyojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) na Halmashauri
ya Manispaa ya Shinyanga
Post Top Ad
Your Ad Spot
Wednesday, March 23, 2022
Home
KITAIFA
CHOO CHA KISASA CHA UMMA NA MTAMBO WA GESI ASILIA VYAZINDULIWA KITUO CHA MABASI SHINYANGA
CHOO CHA KISASA CHA UMMA NA MTAMBO WA GESI ASILIA VYAZINDULIWA KITUO CHA MABASI SHINYANGA
Tags
KITAIFA#
Share This
About kilole mzee
KITAIFA
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment