MEYA wa Jiji la Arusha
Maximillan Iranqe amewataka waganga wanaojishughulisha na tiba asilia
mkoani Arusha kuwekeza zaidi katika tafiti za mimea inayotibu maradhi ya
mbalimbali kama nchi za barani Asia hususani China.
Pia
awashauri waganga hao kujiepusha na vitendo vya utapeli ili kuipa sifa
na hadhi taaluma hiyo tofauti na inavyozungunzwa kwa sasa.
Akizungumza
kwenye mkutano wa halmashauri kuu ya Chama Cha Waganga na wakunga wa
Tiba asilia(Chawatiata) kilichofanyika katika ofisi za Ccm wilayani
Arusha amewataka waganga hao kufikiria kuwekeza nguvu zaidi kwenye ubora
wa dawa mbalimbali hususani mitishamba inayotibu maradhi mbalimbali.
"Fikirieni
kuwekeza kwenye ubora wa madawa yenu hususani mitishamba kama
wanavyofanya nchi za Asia kama China," amesema na huku akiwataka pia
washiriki washiriki wa mkutano huo kuepuka vitendo vya utapeli na
udanganyifu ili kuipa sifa taaluma hiyo.
Aidha amewashauri
kuboresha mazingira ya maeneo wanayofanyia kazi pamoja na bidhaa
wanazowapa wagonjwa."Lazima mjipambanue baina ya waganga wa kienyeji na
tiba asilia acheni kufunga dawa kwenye magazeti lakini muwe
smart(nadhifu)" amesema Meya Iranqe
Kwa upande wake Makamu
Mwenyekiti wa Chama hicho Kiondo Msangi amemwambia Meya huyo aliyekuwa
mgeni rasmi kwenye mkutano huo kuwa chama chao mbali na kisajiliwa
kisheria na kupewa leseni ya uendeshaji lakini wamekuwa wakifanya kazi
kwenye mazingira magumu kutokana na baadhi ya wanachama kukamatwa hovyo
na kutozwa adhabu kinyume na sheria.
Msangi amesema kuna kikundi
cha baadhi ya watu kimekuwa kikizunguka mkoani Arusha na kuwashawishi na
kuwapotosha wajumbe kutojiunga na chama hicho kutokana na sababu zao
binafsi na kuiomba serikali kukichukulia hatua.
Wakati huo huo
,Katibu wa chama hicho ,Kifumba Mkombozi amesema kwamba chama chao
kimekuwa kikishirikiana na serikali katika kuwafichua wapiga ramli
chonganishi,majambazi na hata kukemea mauaji na watu wenye ulemavu wa
ngozi na kuiomba serikali kuwaunga mkono.
Awali Kaimu Mganga Mkuu
wa Hospitali ya Mkoa wa Arusha (Mt Meru),Dk.Omary Chande ametoa rai kwa
waganga hao kuhakikisha wanawakamata wale wanaofanya shughuli za tiba
asilia bila leseni kwa kuwa hao ndio wanachafua taaluma hiyo.
Dk.
Chande ameshauri waganga hao kuhakikisha wanashiriki kikamilifu na
kuunga mkono na kuhamasisha zoezi la chanjo ya Uviko -19 linaloendelea
nchini kwa kuwa wao wana nafasi kubwa ndani ya jamii.
Meya wa Jiji la Arusha Maximillan akizungumza kwenye Mkutano huo uliohusisha waganga wa tiba asili mkoani Arusha
No comments:
Post a Comment