Na Anthony Ishengoma-Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Dkt Philemon Sengati amewataka wachimbaji wadogo wa mgodi wa Nyandorwa
ulioko Solwa Wilaya ya Shinyanga kutambua kuwa wakati wanatafuta kukuza
uchumi kupitia biashara na uchimbaji madini ya dhahabu ni lazima
kuhakikisha usalama wa watu unazingatiwa kwa asilimia miamoja.
Dkt
Sengati amsema hayo leo alipofika katika mgodi huo kujionea zoezi la
kuwakwamua watu walionasa katika duara namba nne ambalo kwa siku mbili
zilizopita liliporomoka na kufukia baadhi ya wachimbaji mgodini hapo na
kusifu juhudi ambazo zimefanyika kunusuru maisha ya wachimbaji sita
waliokuwa wamenasa katika kifusi hicho.
Aidha Dkt. Sengati
aliwapongeza wachimbaji kwa juhudi zao za kuendelea kuchimba udongo
katika eneo la ajali kwa lengo la kutaka kujiridhisha kama bado kuna mtu
ambaye bado amenasa katika duara hilo.
Mkuu wa Mkoa
aliwakumbusha kuwa watu hao ni watanzania na ni rasimali mali muhimu
ambayo bado inahitajika na kwamba bila watu hawa rasilimali ya madini
haiwezi kusaidia katika kutumia utajiri huu tuliojaliwa na Mungu na
kuwataka kuendelea kijiridhisha ili hatimaye waweze kuona kama kuna
aliyebaki chini ya duara na kuendelea na kazi za kukuza uchumi.
‘’Ndugu
zangu haya yaliyojitokeza yakawe shamba darasa tufanye tahimini ya haya
yaliyojitokeza na tukague maeneo yetu ili kubaini kama kuna dalili za
kudondoka kama ilivyotokea hapa na kuyawekea alama za
hatari.’’Aliendelea kusisitiza Dr. Sengati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Awali
mchimbaji mdogo aliyenasuriwa katika kifusi cha duara hilo Toga Lukaga
mkazi wa Malinyi Mkoani Morogoro aliimbia kamati ya ulinzi na usalama ya
Mkoa wa Shinyanga ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kuwa ajali
hiyo ilitokea tare 15 mwezi huu wakati yeye na wenzake watano walipozama
katika duara hilo kwa ajili ya kuanza kazi.
Bw. Lukaga
alibainisha kuwa wakiwa ndani ya duara walibaini kuwepo kwa nyufa katika
dura hilo ndipo alipowaambia wanzake kwamba waondoke katika eneo hilo
lakini wakiwa bado wanatafakari ndipo duara hilo lilipoanza kuporomoka.
Lukaga
aliendelea kusema kuwa yeye na wenzake watatu walibahatika kujinisuru
na kati yao wawili walibanwa na kifusi na mmoja kukatika mguu na
mwingine mkono na kuongeza kuwa mfanyakazi mwenzao aitwaye Burugu
Clement hawajafanikiwa kumuona mpaka sasa kwani katika harakati za
kujiokoa alikimbilia katika njia yake tofauti na wao.
Naye Bw.
Abubakary Magesa ambaye kwa vyeo vya uongozi wa Mgodi ni Inspekta
alisema pamoja na wafanyakazi waliokuwa wanafanyakazi chini ya duara
inspekta wenzake watatu waliofika eneo la hilo duara kuangalia
kilichokuwa kinaendelea ili kutoa msaada nao waloporomoka pamoja na
kifusi lakini waliokolewa na kufanya idadi ya waliookolewa kuwa sita.
Aidha
Frank Bundala ambaye pia ni kiongozi katika mgodi huo aliongeza kuwa
awali kazi ya uokozi ilikuwa ngumu kutoka na uwepo wa kifusi kikubwa
lakini baada ya kutumia gereda kutoa kifusi hicho sasa wamepata njia ya
kuendelea chini zaidi ili waweze kujilidhisha kuona kama kuna mtu yeyote
ambaye bado amenasa chini ya duara hilo.
Mkuu wa Wilaya ya
Shinyanga Bi. Jasinta Mboneko aliutaka uongozi wa mgodi huo kuhakikisha
wanakuwa na takwimu sahihi za watu watakao kuwa wanaingia ndani ya duara
kwa ajili ya kuchimba madini ili kuondoa sintofahamu au kuwa na idadi
sahihi na majina wakati tatizo kama hili litakapojitokeza katika siku za
usoni.
Wachimbaji hao wanaendelea kuchimba eneo hilo na kutafuta
njia nyingine zinazoingiliana na duara hilo chini kwa chini ili kubaini
kama bado kuna aliyekwama katika duara ili na baada ya zoezi hilo
kukamilika wataendelea na shughuli zao kama kawaida.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt Philemon Sengati akiongoza kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa kuelekea eneo la lilipo duara namba nne lililoporomoka nakujionea zoezi la uokozi linavyoendelea kujiridhisha kama bado kuna watu waliokwama ndani ya duara hilo.
Mwonekano wa duara namba nne baada ya wachimbaji wadogo wa Mgodi wa Nyandolwa kutoa kifusi na kuendelea na zoezi la uokoaji watu baada ya duara namba nne kuporomoka.
Baadhi ya wachimbaji wadogo wa mgodi wa Nyandolwa ulioko Solwa Wilaya ya Shinyanga wakifuatilia jambo wakati kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa alipofika katika mgodi huo kuwapa pole kufuatia kuporomoka kwa duara namba nne la mgodi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt Philemon Sengati akipunga Mkono kuongea wachimbaji wadogo wa mgodi wa Nyandolwa ulioko Solwa Wilaya ya Shinyanga jana alipofika katika mgodi huo kuwapa pole kufuatia kuporomoka kwa duara namba nne la mgodi huo.
No comments:
Post a Comment