A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, September 18, 2021

CCM YASHUSHA MAELEKEZO MAZITO BANDARI YA MTWARA,WIZARA YA AFYA

Na Mwandishi Wetu,Mtwara

KATIBU  wa Halmashuri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka ametoa  maagizo kwa Uongozi wa Bandari ya Mtwara ikiwemo kuhakikisha  bandari hiyo kuanza  kutoa huduma za  haraka ili kuzalisha ajira, kuchochea uchumi wa Mtwara na nchi pia.

Pia ameitaka mamlaka hiyo ya bandari kuweka mkakati thabiti wa kuitangaza bandari hiyo ili wafanyabiashara na wawekezaji mbalimbali waijue na waitumie kuingiza na kusafirisha mizigo yao.

Akitoa maagizo hayo leo, Septemba17  2021, Shaka akiwa Wilayani Mtwara ikiwa ni muendelezo wa ziara ya wajumbe na sekretariet inayoongozwa na Katibu Mkuu Daniel Chongolo.

Amesema pamoja na uwekezaji  Mkubwa uliofanyika katika bandari hiyo  wa takribani bilioni 158.8  za kuboresha ni ajabu haitoi huduma kama ilivyokusudiwa. "Sababu ikiwa ni urasimu na hata hujuma zinazofanywa na baadhi ya watendaji wa kiserikali kwa kushirikiana na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu," amesema Shaka

Amesema Chama chao hakitakubali  kuona utekelezaji wa ilani yao ya uchaguzi unakwamishwa kwani kufanya hivyo ni kumkwamisha Rais  Samia Suluhu Hassan na kuchelewesha maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

"Haiwezekani Rais Samia amemtuma Waziri Mkuu Majaliwa lakini baadhi ya watendaji wasiwaminifu wamepuuza maagizo hayo kamwe CCM haitamvumilia  yoyote mwenye nia ovu ya kukwamisha jitihada za Rais Samia katika kuwaletea maendeleo watanzania atakwama yeye,"amesema  Shaka  Mwenezi Taifa

Wakati huo huo Shaka   ameitaka Wizara ya Afya kuacha sinema za maonesho kwa kutoa maelekezo na ahadi zisizotoa matokeo yanayopimika na kuonekana kwa wananchi.

"Naitaka wizara ya Afya kueleza kama walimdanganya Makamu wa Rais wa  Tanzania  Dkt Philip Mpango alipofika kuweka jiwe la msingi mapema mwezi Oktoba katika  Ujenzi wa hospital  ya kanda Mtwara inayogharimu takribani bilioni 15, ambapo walimwambia kuwa  itakuwa imeanza kutoa huduma lakini ajabu mpaka leo hakuna dalili hizo. "amesema na kuongeza

"Sasa ni vizuri wabadilike waanze kuwa watendaji badala ya kuwa wapiga maneno matupu...pamoja na kasi nzuri ya ujenzi inayofanywa na mkandarasi ambaye ni shirika la Nyumba la Taifa, wizara  hiyo  imekuwa kikwazo kikubwa katika kuhakikisha hospitali hiyi inakamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi,"amesema



 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages