Na Leandra Gabriel, Mexico | MWANASIASA
Maarufu nchini Mexico Carlos Mayorga ameingia katika mijadala
mbalimbali baada ya kuzindua kampeni zake za Ubunge akiwa ndani ya
jeneza France24 imeripoti.
Carlos
Mayorga alitumia njia hiyo kuonesha hali halisi ya taifa hilo ambalo
mamia ya watu wanakufa kutokana na virusi vya Corona pamoja na vurugu
zinazohusiana na biashara.
Akiwa
mgombea kutoka chama cha Encuentro Salidario kusini mwa jimbo la
Chihuahua Mayorga alisema, alifikia uamuzi huo kwa malengo ya kufikisha
ujumbe kwa wanasiasa ambao wanasababisha watu kupoteza maisha kutokana
na kutojali kwao.
Mwanasiasa
huyo aliwasili katika kampeni zake katika daraja linalotengenesha mji
wa wa Ciudad Juarezy na El Paso Texas akiwa ndani ya jeneza la rangi ya
fedha.
Carlos
Mayorga aliambatana na wasaidizi waliovaa mavazi na vifaa vya kujilinda
wakiwa na mashada ya maua kama ishara ya kupaza sauti juu ya janga hilo
ambapo hadi sasa watu 200,000 wamefariki nchini humo kutokana na
Covid-19.
Vyombo vya habari vilimnukuu mwanasiasa huyo akisema;
"Wanasiasa
wameendelea kukaa kimya wakati matukio ya uhalifu yakiendelea, na
wameendelea kukaa kimya kuhusu hali mbaya ya Covid-19." Alinukuliwa.
Zaidi
ya watu 300,000 wameuawa nchini Mexico tangu Serikali itoe nguvu kwa
jeshi katika kupambana na vita dhidi ya dawa za kulevya 2006 kwa mujibu
kwa taarifa rasmi.
No comments:
Post a Comment