Mkurugenzi
wa M-Pesa, Epimack Mbeteni (katikati), Afisa Mtendaji Mkuu wa Britam
Tanzania, Raymond Komanga (kushoto) na Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti
wa TIRA, Zakaria Muyengi (kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja mara
baada ya uzinduzi wa huduma mpya ya VodaBima (Bimika Kidijitali)
itakayowezesha mteja kulipia bima kwa simu ya mkononi kupitia M-Pesa.
Uzinduzi huu umefanyika leo jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi
wa M-Pesa, Epimack Mbeteni akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma mpya
ya VodaBima (Bimika Kidijitali) itakayowezesha mteja kulipia bima kwa
simu ya mkononi kupitia M-Pesa. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar
Es Salaam.
Mkurugenzi
wa Masoko na Utafiti wa TIRA, Zakaria Muyengi akizungumza kwenye
uzinduzi wa huduma mpya ya VodaBima (Bimika Kidijitali) itakayowezesha
mteja kulipia bima kwa simu ya mkononi kupitia M-Pesa. Uzinduzi huo
umefanyika leo jijini Dar Es Salaam.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Britam Tanzania, Raymond Komanga ( kushoto )
akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma mpya ya VodaBima (Bimika
Kidijitali) itakayowezesha mteja kulipia bima kwa simu ya mkononi
kupitia M-Pesa. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar Es Salaam.
Jukwaa
la kidijitali linalowezesha upatikanaji wa huduma za bima kwa urahisi
zaidi na za bei nafuu kwa kushirikiana na kampuni ya Britam Tanzania.
Zaidi ya wateja milioni 13 wa M-PESA kupata Bima ya Magari kupitia simu zao
Aina zingine za huduma za Bima kuongezwa katika orodha ya huduma.
Tarehe
12 Aprili 2021. Dar es Salaam. Kampuni inayoongoza ya Teknolojia na
Mawasiliano nchini, Vodacom Tanzania leo imetangaza kuzindua ‘VodaBima’ –
huduma ya kidijitali itakayowapa wateja huduma ya bima kupitia M-Pesa
na hivyo kuchochea matumizi ya huduma za bima kwa Watanzania kwa kutumia
huduma hiyo kwa njia ya kidijitali.
Kulingana
na ripoti ya Finscope 2013, matumizi ya Bima nchini ilikuwa asilimia
13.0 ikiwa imeongezeka kutoka kutoka asilimia 6.8 2009. Pamoja na ukuaji
huu, bima bado ni moja ya huduma za kifedha ambazo hazitumiki sana
nchini. Sababu tofauti zinatajwa ikiwa ni pamoja na mwamko mdogo,
kutokuaminika kwa huduma na vikwazo vya kupata huduma. Kama kampuni ya
teknolojia iliyo na maono ya kuibadilisha Tanzania na kubadilisha maisha
kupitia teknolojia, Vodacom inapenda kuziba pengo hili kwa kutoa
suluhisho la kidijitali ambalo litarahisisha upatikanaji wa bidhaa za
Bima.
Akizungumza
Jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni alisema
kuwa VodaBima ni nyongeza mpya kwa jalada la M-Pesa la bidhaa na huduma
zote zinalenga kufanya ujumuishaji wa kidijitali nchini Tanzania uwe wa
kweli.
“Kwa
miaka 13 sasa, Vodacom M-Pesa imekuwa kichocheo muhimu katika ukuaji wa
ujumuishaji wa kifedha nchini na kila wakati tunatafuta njia mpya za
kushinikiza uchumi jumuishi wa kidijitali. Vodacom inakusudia kuziba
pengo la upatikanaji wa huduma za bima kwa kutoa suluhisho la kidijitali
ambalo litapunguza gharama na kuongeza upatikanaji wa bidhaa za Bima."
VodaBima
huwapa wateja fursa ya kujiwekea akiba ya Bima bila malipo katika mkoba
wao wa VodaBima kwa mwaka mzima. Jukwaa la VodaBima litatuma taarifa za
kumbukumbu kupitia SMS wakati Bima ya gari yako inakaribia kuisha.
Bwana
Mbeteni ameongeza kuwa bidhaa hiyo mpya italeta huduma za bima karibu
na wateja na kuongeza urahisi na upatikanaji wa huduma hiyo. Aliongeza
kuwa huduma hiyo itakuza sekta ya bima nchini kwa ujumla. VODABIMA
inatumia miundombinu bora ya teknolojia ya M-Pesa na mtandao mpana wa
Vodacom ambayo inapatikana katika maduka Vodacom nchini kote
kuhakikisha usalama, urahisi wa upatikanaji wa huduma za bima.
“VodaBima
ni huduma ya kwanza ya aina yake sokoni, huduma hii inarahisisha
upatikanaji wa huduma za bima pamoja na mfumo wa kufanya madai. Kwa sasa
tunatoa bima ya gari lakini tunapanga kuleta bidhaa zingine ili kukidhi
mahitaji ya wateja na kwenda sambamba na mabadiliko ya soko,” alisema Mbeteni.
Mkurugenzi
wa Masoko na Utafiti kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Bima Tanzania –
TIRA, Zacharia Muyengi alisema kuwa kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma
za bima kupitia simu za mkononi kutawanufaisha wateja zaidi kwani sasa
watafahamu kwa kina huduma mbalimbali za bima zinazotolewa sokoni.
“Tunafanya
kazi kukuza na kudumisha soko la bima linalojumuisha, lenye ufanisi, la
haki na salama kwa faida na ulinzi wa wamiliki wa sera. Tunakaribisha
matumizi ya teknolojia ya mawasiliano pamoja na ubunifu wa bidhaa ili
kuleta huduma hizi karibu na watu. Uzinduzi wa VodaBima ni hatua
inayoelekea kuboresha huduma ya bima nchini,” alifafanua Muyengi.
Kwa
upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Britam Tanzania Raymond
Komanga ambao wanashirikiana na Vodacom kusambaza huduma ya bima kupitia
teknolojia ya kidijitali alisema kuwa matumizi ya teknolojia ya
mawasiliano ya simu katika kupata bima ni hatua itakayofanya huduma hiyo
ipatikane kwa watu wengi zaidi. Aliongeza kwamba huduma hiyo itasaidia
kuhamasisha watu wengi zaidi kutumia huduma ya bima na kukuza sekta
hiyo kwa ujumla.
“Huduma
ya VodaBima ni ya kimapinduzi kwa sababu italeta urahisi kwa wateja
kupata huduma za bima kutoka kwa watoa huduma. Wateja hawatalazimika
kutembelea kampuni za bima kwani wanaweza kupata huduma hiyo kupitia
simu zao za mkononi,” alisema Komanga huku akiongeza kwamba jamii itaelimika zaidi juu ya bidhaa na manufaa ya utumiaji wa huduma za bima.
Uzinduzi
wa VodaBima ni sehemu ya mpango wa ujumuishaji kupitia teknolojia ya
kidijitali ya kampuni ya Vodacom na hatua nyingine zaidi katika kuleta
huduma karibu na wateja kupitia ubunifu na teknolojia ya mawasiliano
kupitia simu za mkononi.
“Tunataka
wateja wetu wapate huduma ya bima iliyoimarishwa pande zote. VodaBima
ni bidhaa ya ziada ambayo inaweza kupatikana kupitia zana (App) mpya ya
M-Pesa ambapo wateja wanaweza kupata bidhaa zingine kama huduma za
mikopo na akiba kama Songesha na M-Pawa,” alihitimisha Mbeteni.
Uzinduzi
wa VodaBima ni sehemu ya mpango wa ujumuishaji kupitia teknolojia ya
kidijitali ya kampuni ya Vodacom katika kuleta huduma karibu na wateja
kupitia ubunifu na teknolojia ya mawasiliano kupitia simu za mkononi.
No comments:
Post a Comment