Naibu
Waziri wa maji Maryprisca Mahundi kulia akifungua koki katika mradi wa
maji wa Kipapa na Mhilo uliotekelezwa na wakala wa maji vijijini Ruwasa
mkoa wa Ruvuma ambao umewezesha wakazi wa kijiji cha Kipapa katika
halmashauri ya wilaya ya Mbinga kuondokana na kero ya maji safi na
salama iliyokuwepo kwa muda mrefu.
Naibu
Waziri wa Maji MaryPrisca Mahundi amefanya ziara ya kikazi Wilayani
Mbinga mkoani Ruvuma kwa kukagua miradi ya maji ya mabilioni ya fedha.
Katika
ziara hiyo Mahundi amekagua mradi wa maji wa Kipapa na Mhilo ambao
umetekelezwa kwenye Kata za Kipapa na Langiro, Halmashauri ya Wilaya ya
Mbinga wenye thamani ya shilingi Milioni 647.4
Mradi huo umekamilika na umeanza kuhudumia wananchi kwa kutoa maji safi na salama.
Naibu
Waziri wa Maji pia ametembelea na kukagua miradi mingine miwili ya maji
ambayo ni mradi katika Kijiji cha Lifakara unaokadiriwa kugharimu
Shilingi Milioni 651 na mradi unaojengwa Kata ya Bethlehemu ambao
unatarajia kugharimu sh.Bilioni 1.4 hadi kukamilika kwake.
Katika
ziara hiyo Naibu Waziri wa maji pia amekagua miradi ya maji
inayotekelezwa kwenye vijiji vya Amani Makolo, Mabuni, Luhagara na
Litumbandyosi wilayani Mbinga.
Akizungumza
baada ya kukagua miradi hiyo Naibu Waziri wa Maji ametoa mwezi mmoja
kwa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Ruvuma(RUWASA)
kuongeza vituo vya kuchotea maji kwenye kitongoji cha Kiosi, Kijiji cha
Kipapa.
“RUWASA
hakikisheni mnaanza utekelezaji wa mradi wa kusambaza maji kwenye
Kijiji cha Langiro Asili, Kata ya Langiro ndani ya kipindi cha miezi
mitatu ijayo’’, alisisitiza Mahundi.
Kwa
upande wake Meneja wa RUWASA Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Rebman Ganshongwa
ametoa rai kwa wananchi kutunza vyanzo vya maji sanjari na miundominu ya
maji iliyopo kwenye maeneo yao ili miradi hiyo iweze kudumu kwa muda
mrefu na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
No comments:
Post a Comment