A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, April 28, 2021

HUDUMA YA MAMA NA MTOTO YATAKIWA KUWEPO KATIKA NGAZI ZOTE ZA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA NCHINI

 

Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima akiwa amebeba mtoto Mourine na pembeni ni mama wa mtoto huyo ambaye amepatiwa chanjo.

Dkt.Gwajima akiwa amembeba mtoto ambaye amewakilisha Watoto wote nchini kupata Chanjo kwa ajili ya kumkinga na Magonjwa yanayozuilika kwa Chanjo.


Mtoto Mourine Samweli mwenye umri wa miezi sita akiwa amebebwa na mama yake Bi.Emmanuela Ramadhani mkazi wa Mazimbu Manispaa ya Morogoro akiwa tayari kupatiwa chanjo Kwenye viwanja vya Chamwino Kwenye maadhimisho ya wiki ya chanjo Kitaifa yaliyofanyika mkoani Morogoro.

Akina Mama wa Manispaa ya Morogoro wakiwa na Watoto wao tayari kwa kupatiwa chanjo kulingana na umri.



Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Locate Ile Sanare akizungumza na wakazi wa manispaa ya Morogoro.

Mwakikishi wa Umoja wa Mataifa (UN) Dkt. William Mwengee akitoa salamu kwa niaba ya  mashirika ya kimataifa Kwenye maadhimisho hayo.



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Dorothy Gwajima akishangiliwa na wanafunzi wa shule ya msingi Chamwino A na B wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya chanjo duniani.

Na.Catherine Sungura,WAMJW-Morogoro

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima ameagiza majengo yote ya vituo vya kutolea Huduma ambayo bado hayajaanza kutoa Huduma za afya kote nchini kuanza Mara moja kutoa Huduma za mama na mtoto ikiwemo utoaji wa chanjo ili kupunguza changamoto za afya.

Dkt. Gwajima ameyasema hayo leo mkoni Morogoro wakati akifungua maadhimisho ya wiki ya chanjo ambayo Kitaifa yamefanyika Kwenye viwanja vya Chamwino.

Dkt. Gwajima amesema kuwa yapo majengo mengi yamejengwa lakini hayajaanza kutoa huduma za Magonjwa ya nje (OPD) na kuagiza yaanze Sasa kutoa huduma za mama na mtoto ikiwemo Chanjo ili kuwapunguzia mwendo mrefu akina mama wajawazito na Watoto.

Kwa upande wa maadhimisho ya wiki ya Chanjo Dkt. Gwajima amesema madhumuni ya wiki hii ni kuhamasisha na kuelimisha Jamii kuhusu umuhimu wa huduma za Chanjo Katika kukinga Magonjwa yanayozuilika kwa Chanjo na kuepusha vifo vinavyoweza kuzuilika kwa Chanjo.

"Ninawahimiza familia kuwapeleka Watoto wote  wanaostahili kupata Chanjo Katika vituo vinavyotoa huduma za afya vya Serikali na binafsi ili Watoto wapate chanjo".

Aliongeza kuwa chanjo ni mkakati muafaka Katika kutokomeza Magonjwa na kupunguza vifo hususan vya Watoto wa chini ya miaka mitano na hivyo kupunguza gharama kubwa ambazo familia zetu na Taifa kwa ujumla ingetumika Katika kutibu maradhi yatokanayo na Magonjwa yanayozuilika kwa Chanjo.

Dkt. Gwajima aliyataja Magonjwa yanayokingwa  ni pamoja na Kifua Kikuu,Dondakoo, Kifaduro, Polio, Surua, Rubella, Pepopunda, Hima ya Ini, Homa ya Uti wa Mgongo,Pepopunda,Nimonia/Kichomi, Kuhara na Saratani ya mlango wa kizazi.

"Chanjo huzuia takribani vifo milioni 2 Hadi 3 kila mwaka kutokana na maradhi yanayozuilika kwa Chanjo duniani,na hapa nchini mafanikio ya chanjo tumefanikiwa kutokomeza Ndui,Dondakoo,Kifaduro,Polio na Pepopunda na wodi za wagonjwa wa Surua zimefungwa".Aliongeza Dkt. Gwajima

Aidha, ametaja takwimu za hivi karibuni zinaonesha kwa miaka mitano mfululizo kiwango Cha uchanjaji Kitaifa ni zaidi ya asilimia 95 na hivyo kuifanya Tanzania  kuwa miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri Katika utoaji wa huduma za Chanjo.

"Kiwango hiki Cha uchanjaji hapa nchini pamoja na Afua zingine na kuwezesha nchi kufikia lengo Namba 4 la Malengo ya Mikenia(SDG 4) kwa kupunguza vifo vya Watoto chini ya umri wa miaka mitano kwa theluthi 2/3".

Hata hivyo Dkt. Gwajima alisisitiza kila mwananchi anawajibu wa kuhakikisha mtoto wake mtoto wa jirani ambaye hajapata  au kukamilisha chanjo anapata chanjo kulingana na ratiba kwani mtoto asiyepata chanjo ni hatari kwa afya yake na afya ya Jamii inayomzunguka sababu  anaweza kuambukizwa Magonjwa na kuambukiza wengine sababu ya kukosa Kinga.

Maadhimisho ya wiki ya chanjo huadhimishwa kila mwaka kuanzia tarehe 24 Hadi 30 Aprili na kauli mbiu ya mwaka huu inasema "Jamii iliyokingwa, Jamii yenye afya Bora" .

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages