A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, April 16, 2021

Dkt. Abbasi Awapiga Msasa Waandishi Wa Habari Za Mtandaoni

 

 
………………………………………………………………………………
Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amewataka Waandishi wa Habari nchini  kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kuepuka makosa ya kisheria yanayoweza kujitokeza.
Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo jijini Dodoma alipokuwa akitoa mada juu ya ”Matumizi ya Mitandao ya Kijamii”’ wakati wa mafunzo kwa Waandishi wa Habari za mtandaoni wa Shirika la Utangazaji Tanzania  (TBC) (TBConline).
Amewataka kutojiona wanyonge kwa kufanya kazi hiyo,  bali wajione watu waliobeba dhamana kubwa katika kuihabarisha jamii mambo mbalimbali yanayoendelea duniani.
“Si lazima Waandishi wote wa Habari waonekane kwenye Televisheni, kuna namna nyingi za kufanya kazi hii ikiwemo mitandao ya kijamii ambayo watumiaji wake wanaongezeka kwa kasi, kwa sasa dunia imehama kutoka mtaani kwenda mtandaoni.”  amefafanua Dkt. Abbasi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages