Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Bw Gullamhussein Kifu (watatukushoto) akipokea msaada wa madawati viti pamoja na meza 500 kwa ajili ya shule za wilaya hiyo kutoka kwa Mkurugenzi wa Wateja wa wadogo wa Benki ya NBC Bw Elibariki Masuke(wa pili kulia) msaada huo ukilenga kuboresha sekta ya elimu Wengine pichani ni Mbunge wa jimbo la Kibiti Bw Twaha Mpembenwe (kushoto),Mkurugenzi wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC Bi Neema Singo (wa pili kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kibiti Bw Abduljabir Marombwa hafla hiyo imefanyika hivi karibuni wilayani kibiti.
Mkurugenzi wa Wateja wa wadogo wa benki ya NBC Bw Elibariki Masuke akizungumza na wajasiriamali wanawake wilayani Kibiti wakati wa mafunzo ya kibiashara na ujasiriamali kwa wanawake wajasiriamali 150 wilayani humo ili kuwajengea uwezo wa kuemdesha biashara zao kwa ufanisi huku wakizingatia nidhamu ya fedha kabla hawajapatiwa mikopokwa ajili ya kukuza mitaji yao na benki hiyo.Kibiti, Pwani: April
17, 2021: Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imetoa msaada wa madawati 250, viti
viti pamoja na meza 250 wilayani Kibiti mkoni Pwani ikiwa ni sehemu ya Mpango
wa kipekee wa uwajibikaji wa Jamii (CSR) ambao unaplenga kuchangia utoaji wa elimu
bora nchini.
Zaidi, benki hiyo pia imetoa mafunzo ya kibiashara na
ujasiriamali kwa wanawake wajasiriamali
150 wilayani humo ili kuwajengea uwezo wa kuemdesha biashara zao kwa ufanisi
huku wakizingatia nidhamu ya fedha kabla hawajapatiwa mikopokwa ajili ya kukuza
mitaji yao.
Madawati hayo yalikabidhiwa na Mkurugenzi wa Idara ya wateja
wadogo wa benki hiyo Bw Elibariki Masuke wakati wa hafla fupi ya makabidhiano
iliyofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya Hiyo Bw Gullamhussein Kifu . Hafla
hiyo pia ilihudhuriwa na Mbunge wa jimbo la Kibiti Bw Twaha Mpembenwe pamoja na
maafisa wengine wa wilaya hiyo akiwemo
Mkurugenzi Mtendaji.
Bwana Masuke alisema kuwa benki hiyo imejitolea kusaidia
katika kuboresha ustawi wa jamii kupitia misaada ya kijamii ikiwemo elimu na
kwamba wameguswa sana na suala la changamoto ya madawatikwenye baadhi ya maeneo
hapa nchini sababu iliyosababisha wao kuchukua hatua hiyo ili kuboresha zaidi sekta hiyomuhimu.
"Ni furaha kwetu kuwa sehemu ya kutatua changamoto
kwenye sekta muhimu kama hii. Kupitia ushirikiano na ushawishi tunaoupata
kutoka kwa Mbunge wa Kibiti na ofisi ya Mkuu wa wilaya tunaahidi kuendelea
kushirikiana na jamii ya wana Kibiti huku pia tukifikiria namna kufungua tawi
letu wilayani Kibiti kufuatia fursa
mbalimbali tunazoziona ikiwemo kilimo na mradi wa kituo cha kupozea umeme wa
Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere,’’ alisema.
Alishauri pia wanafunzi na walimu watakaonufaika na msaada
huo kutunza madawati na meza hizo ili viweze kutumika kwa muda mrefu na hivyo
kusaidia walengwa wengi zaidi.
Kuhusu mafunzo kwa wajasiriamali wanawake Bwana Masuke alisema kuwa miongoni mwa sababu
zinazokwamisha utoaji wa mikopo kwa wajasiriamali wengi ni pamoja na wao
kuendesha biashara zao bila kuzingatia misingi ya kifedha ikiwemo kutunza
kumbukumbu za mahesabu ikiwemo mapato na matumizi.
Kwa mujibu wa Bw Masuke ni kutokana na uwepo wa changamoto
hiyo ndio sababu benki hiyo imekuwa ikishirikiana na taasisi nyingine ikiwemo
TanTrade, SIDO, VETA na washauri binafsi kuelimisha wajasiriamali kuhusu namna
bora ya kusimamia na kuendesha biashara zao ili kuwajengea uwezo kabla ya
kuwapatia mikopo.
"Tumekuwa tukishirikiana na washirika wengine kutoa
mafunzo kwa wajasiriamali na wafanyabiashara kwenye maeneo kama usimamizi wa
hesabu, utunzaji wa vitabu na uongozi, ili tuwaweke vizuri kwa ufikiaji rahisi
wa mikopo", Masuke alisema.
Akizungumza mara tu baada ya kupokea msaada huo Mkuu wa
Wilaya ya Kibiti Bw Gullamhussein Kifu pamoja na kuishukuru benki ya NBC kwa
kutoa msaada kwa wakati haswa unaohitajika, aliiomba benki hiyo ifungue tawi
lake wilayani humo mapema iwezeknavyo ili iweze kuwasaidia wakulima na
wafanyabiashara husani wadogo.
"Msaada huu utasaidia kupunguza changamoto ya uhaba wa
madawati katika baadhi ya shule zetu…tunashukuru sana NBC tunaomba muendelee
kusaidia kwenye maeneo mengine pia ikiwemo sekta ya afya ." Alisema.
Akizungumzia mafunzo kwa wajasiriamali wanawake wilayani
humo Bw Kifu alitoa wito kwa washiriki kuhakikisha wanayatumia vyema kwa kuwa
yanalenga kuwasaidia katika upatikanaji wa mikopo sambamba na kuendesha biashara
zao kwa ufanisi na kwa faida
“Kibiti ni wilaya changa inayohitaji watu wake ili kuendelea. Kabla hatujapokea wawekezaji kutoka nje ni lazima tuanze sisi wenyewe humu ndani. Kupitia mafunzo haya tunakwenda kupata wajasiriamali na wafanyabaishara wenye weledi wa kutosha kutambua fursa zilizopo na kuzitumia,’’ alisema.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo hilo Bw Twaha Mpembenwe
aliiomba benki hiyo iendelee kuwekeza zaidi wilayani humo kwa kufungua tawi
lake sambamba na kuwasaidia wajasiriamali na wakulima hususani wa zao la ufuta
pamoja na vijana ambao kwasasa wanakibiliwa na changamoto ya huduma za
kifedhaikiwemo mikopo na elimu ya biashara na kilimo cha kisasa.
No comments:
Post a Comment