A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, June 17, 2020

KLABU YA YANGA YAMTOZA FAINI YA SHILINGI MILIONI MOJA BEKI WAKE




Klabu ya Yanga imesema itamkata Shilingi Milioni moja (1,000,000) kutoka  kwenye mshahara wake, beki wake Lamine Moro kwa kitendo cha kumkanyaga mchezaji wa JKT Tanzania Mwinyi Kazimoto.

Uongozi wa timu hiyo umekemea kitendo hicho kilichofanywa na Beki wake huyo kwenye mchezo wa ligi kuu ya Soka Tanzania bara, uliopigwa leo jijini Dodoma na kumuomba radhi Mwinyi Kazimoto, JKT Tanzania na wapenzi wa Soka kwa ujumla.

Tamko hilo la Yanga limetoka takriban dakika 40 mara baada ya mchezo wan a JKT kumalizika ambapo katika Mchezo huo timu zote zilitoshana nguvu kwa kufungana bao moja kwa moja ikiwa timu ya Yanga ikitoka nyuma kwa golo moja kupitiwa Patrick Sibomana katika dakika za lala salama huku goli la JKT Tanzania likifungwa na Michael Aidan.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages