A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, June 17, 2020

RAIS MAGUFULI ACHUKUA FOMU YA KUOMBA KUTEULIWA NA CCM KUGOMBEA NAFASI YA URAIS

Na Said Mwishehe,Michuzi TV.

RAIS Dk.John Magufuli amechukua fomu ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) leo Juni 17,mwaka 2020 katika Makao ya Chama hicho Jijini Dodoma.

Dk.Magufuli anachukua fomu hiyo kwa ajili ya kuomba tena ridhaa ya kugombea nafasi hiyo kwa tiketi ya CCM ikiwa ni awamu ya pili baada ya kumaliza awamu ya kwanza ya miaka mitano iliyoanzia mwaka 2015 mpaka mwaka 2020.Uchuguzi Mkuu mwaka huu unatarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Akizungumza leo Mjini Dodoma baada ya kuchukua fomu hiyo ya kugombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk.Magufuli amesema leo ameona achukue fomu hiyo kwani kwa mujibu wa ratiba ya Chama zimebaki siku 13 za kuchukua na kurudisha fomu.

"Samahani nimewavamia , naomba mnisamehe Mwenyekiti, kutokana na vikao vya Chama zilikuwa zimebaki siku 13, ilikusudi fomu ziwe zimechukuliwa na kurudishwa, basi nimeamka leo nikasema ngoja nikatimize wajibu wangu , wa chama changu, ili nikafanya kazi ya chama changu ambacho kiniliniamini katika miaka mitano.

"Kwa hiyo nimekuja leo asubuhi hapa, nimechukua fomu ilikusudi niweze kuzitembeza kwa wanachama na baada ya kuchukua tu nimejua hapa ni makao makuu na wewe ni Mwenyekiti wa makao makuu ya nchi yetu , ndio maana nimetoka tu kuchukua fomu, nimeona nije hapa kwa ajili ya kupata wadhamini,"amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo amesema kwa taarifa alizonazo kabla ya kufika hapo amepata taarifa kuna wanachama wengi wamejitokeza kumdhamini na tayari kuna majina ya wanachama 25 ambao tayari wamejitokeza.Hivyo ameamua kuacha fomu nyingine kwa ajili ya wadhamini kuajindikisha.

Akiwa kwa Mwenyekiti huyo wa CCM, wanachama wa CCM waliokuwa hapo walianza kuimba wimbo wa Baba Lao.Walikuwa wakiimba hivi "CCM Hoyeeee...Magufuli hoyeee...wataweza kweli? Aaaa wapi...hata wakiungana...hata wakitukana...aaa wapi...maendeleo na Magufuli hoyeee...Magufuli Baba Lao...Magufuli Baba Lao...

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhiwa Fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea Urais kwa Tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadae mwaka huu kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally Kakurwa katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM White House Dodoma leo tarehe 17 JUNI 2020.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka katika Makao Makuu ya CCM White House Dodoma leo tarehe 17 JUNI 2020 mara baada ya kuchukua Fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Urais kwa Tiketi ya CCM

  
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachama wa CCM katika Makao Makuu ya CCM White House Dodoma leo tarehe 17 JUNI 2020 mara baada ya kuchukua Fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Urais kwa Tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadae mwaka huu.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka katika Ofisi ya CCM Makao Makuu ya Mkoa Dodoma mara baada ya kupata wadhamini wa Chama chake cha Mapinduzi CCM. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages