A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, June 15, 2020

CCM Njombe wamnasa Diwani wa kata ya MjiMwema



Na Amiri kilagalila,Njombe

Chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Njombe, kimefanikiwa kumnasa na kumkabidhi kadi ya uanachama aliyekuwa diwani wa kata ya Mjimwema mjini Njombe kupitia tiketi ya CHADEMA Abuu Mtamike huku kikikiri kuwa amewasumbua kwa muda mrefu kama alivyowasumbua aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema mkoa Fakii Lulandala.

Katika kikao cha kumpokea diwani huyo viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi na serikali wamesema bwana Mtamike sasa ameutambua ukweli juu ya kazi kubwa zinazotekelezwa na serikali chini ya Chama tawala.

katibu wa CCM wilaya ya Njombe Hanafi Msabaha anasema sasa viongozi wa CCM kata ya Mjimwema wataweza kumtumia Mtamike kwa shughuli yoyote kwa kuwa hakuna ukakasi tena.

“Kama Mtamike alikuwa hafanyi vizuri nani angeweza kukaa naye na kumrekebisha kwa wakati ule katika chama chake kisichofanya vikao,hakuna kamati za siasa tofauti na Chama cha Mapinduzi,kwa hiyo kwa sasa mnaweza kumfanya mtamike awe vile mnavyotaka”alisema Msabaha.

Akizungumza mara baaa ya kukabidhiwa kadi ya CCM na kula kiapo Abuu Mtamike amesema kilichompeleka Chadema mwaka 2010 sasa kimepatiwa ufumbuzi na Rais Dokta John Pombe Magufuli.

“Tuliingia kama upinzani kwasababu tulikuwa tunataka maendeleo lakini leo yale yote tuliyokuwa tunayataka Dkt,John Pombe Magufuli ametenda”alisema Mtamike

Katibu wa vikao vya kamati ya maendeleo ya kata ambavyo mwenyekiti wake alikuwa diwani Mtamike bwana Augustino Ngailo ambaye ni afisa mtendaji kata ya Mjimwema amemtaka diwani huyo kuacha kuwa kigeugeu baada ya kuingia CCM.

Katibu wa siasa na uenezi wa CCM mkoa wa Njombe Erasto Ngole mbali ya kupongeza uamuzi wa bwana Mtamike kuhamia katika chama hicho lakini ametoa onyo kali kwa wana CCM watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa kuelekea katika uchaguzi mkuu ujao pamoja na wanaotumia fedha zao kuwanyanyasa wengine.

Mwezi Oktoba mwaka huu serikali ya Tanzania inatarajia kuendesha zoezi la uchaguzi mkuu wa Rais,wabunge na madiwani watakaoliongoza taifa kwa miaka mitano ijayo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages