Mkurugenzi Ushirika na Uwajibikaji wa Jamii EMEA na Mkuu wa wiki ya Code Afrika, Claire Gillissen (kulia), akizungumza na Walimu kutoka shule mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kutoa mafunzo ya Programming kwa walimu kutoka Tanzania na Afrika nzima yenyelengo la kukuza elimu mashuleni na na jamii nzima. uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa SAP, Liam Ryan, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kutoa mafunzo ya Programming kwa walimu kutoka Tanzania na Afrika nzima yenyelengo la kukuza elimu mashuleni na na jamii. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Miradi wa taasisi ya Apps and Girls, Jesca Mmari, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kutoa mafunzo ya Programming kwa walimu kutoka Tanzania na Afrika nzima yenyelengo la kukuza elimu mashuleni na na jamii. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwalimu wa shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa akizungumza katika haflahiyo. Picha zote na Brian Peter
Kutokana na umuhimu wa teknolojia katika elimu na jamii kiujumla kuongezeka,Kutokana na umuhimu wa teknolojia katika elimu na jamii kiujumla kuongezeka,Taasisi ya SAP kupitia program ya INITIATIVE CODE WEEKS imeanza kutoa mafunzo ya Programming kwa walimu kutoka Tanzania na Afrika nzima kwa lengo la kuwafikia wanafunzi wengi na kutengeneza msingi mzuri wa teknolojia kwa kizazi cha baadae.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo Mkurugenzi Mkuu wa SAP, Liam Ryan amesema kuwa SAP ikishirikiana na taasisi mbalimbali wamemekusudia kwa dhati kutoa mafunzo kwa walimu zaidi ya mia tano kutoka Tanzania na zaidi ya walimu elfu tano kutoka Afrika wakiwa na lengo la kuwafikia wanafunzi na watoto zaidi ya milioni moja na nusu Afrika nzima.
Kwa upande wake Afisa Miradi wa taasisi ya Apps and Girls, Jesca Mmari amesema kuwa wanakusudia kuwafundisha walimu programu iitwayo scratch ambayo itatoa hamasa na hamu ya wanafunzi kupenda kujifunza teknolojia ambpo amewataka walimu walioko kwenye mafunzo hayo wapende na wajitume kujifunza kuhusu programu hiyo na teknolojia kwa ujumla ili waweze kuwafundisha wanafunzi kikamilifu.
Akizungumza mmoja wa walimu katika mafunzo hayo,Mussa Awadhi kutoka shule ya sekondari Benjaminj Mkapa, amesema kuwa programu ya scratch inamuwezesha mwanafunzi kuelewa kwa urahisi masuala ya teknolojia kwani imetengenezwa kwa mfumo wa picha (katuni)na ni rahisi kujifunzia. imeanza kutoa mafunzo ya Programming kwa walimu kutoka Tanzania na Afrika nzima kwa lengo la kuwafikia wanafunzi wengi na kutengeneza msingi mzuri wa teknolojia kwa kizazi cha baadae.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo Mkurugenzi Mkuu wa SAP, Liam Ryan amesema kuwa SAP ikishirikiana na taasisi mbalimbali wamemekusudia kwa dhati kutoa mafunzo kwa walimu zaidi ya mia tano kutoka Tanzania na zaidi ya walimu elfu tano kutoka Afrika wakiwa na lengo la kuwafikia wanafunzi na watoto zaidi ya milioni moja na nusu Afrika nzima.
Kwa upande wake Afisa Miradi wa taasisi ya Apps and Girls, Jesca Mmari amesema kuwa wanakusudia kuwafundisha walimu programu iitwayo scratch ambayo itatoa hamasa na hamu ya wanafunzi kupenda kujifunza teknolojia ambpo amewataka walimu walioko kwenye mafunzo hayo wapende na wajitume kujifunza kuhusu programu hiyo na teknolojia kwa ujumla ili waweze kuwafundisha wanafunzi kikamilifu.
Akizungumza mmoja wa walimu katika mafunzo hayo,Mussa Awadhi kutoka shule ya sekondari Benjaminj Mkapa, amesema kuwa programu ya scratch inamuwezesha mwanafunzi kuelewa kwa urahisi masuala ya teknolojia kwani imetengenezwa kwa mfumo wa picha (katuni)na ni rahisi kujifunzia.
No comments:
Post a Comment