Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania, Nd. Cosmas Kimario
(wapili kushoto), akikabidhi hundi ya shilingi 495,600,000 kwa Rais wa TFF, Nd.
Wallace Karia, kwa ajili ya udhamini wa Ligi kuu Tanzania Bara. KCB imeendeleza
udhamini wa ligi hiyo kwa msimu wa 2019/20 ikiwa msimu wa tatu mfululizo.
Wanaoshuhudia, (watatu kulia) Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Tanzania, Nd.
John Ulanga, (Mkuu wa Idara ya Masoko wa Benki hiyo Bi. Christine Manyeye na Mwanasheria
Mkuu waBenki ya KCB, Bi. Anthonia Kilama hafla ya makabidhiano hayo imefanyika
leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania, Nd. Cosmas Kimario
(wa tatu kushoto), Pamoja na Rais wa TFF, Nd. Wallace Karia, wakionyesha hundi
ya shilingi 495,600,000 iliyotolewa na benki ya KCB kwa ajili ya udhamini wa Ligi
kuu Tanzania Bara. Benki ya KCB imeendeleza udhamini wa ligi hiyo kwa msimu wa
2019/20 ikiwa msimu wa tatu mfululizo. (watatu kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi
Benki ya KCB Tanzania, Nd. John Ulanga, wengine
ni viongozi kutoka TFF na KCB.
Benki ya KCB Tanzania
imengia mkataba na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ili kuwa
mdhamini mwenza wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara
kwa msimu wa 2019/2020. Mkataba huo wenye thamani ya shilingi za Kitanzania 420,000,000 kabla ya kodi,
ulitiwa saini leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB, Nd. Cosmas Kimario na
Rais wa TFF Nd. Wallace Karia katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es
Salaam.
Benki ya KCB Tanzania
ilidhamini ligi hiyo kwa mara ya kwanza msimu wa 2017/18 kwa thamani ya
shilingi za Kitanzania 325,000,000 na kuongeza udhamini kwa msimu wa 2018/19
kufikia shilingi za Kitanzania 420,000,000. Mafanikio makubwa yaliyopatikana
kwa udhamini wa misimu iliyopita ndiyo yameivutia Benki ya KCB Tanzania
kuendeleza udhamini huo kwa kiasi cha shilingi za Kitanzania 420,000,000
kupelekea jumla ya udhamini ndani misimu mitatu kuwa shilingi za Kitanzania
1.165bn.
Hafla ya kutia saini
makubaliano hayo imehudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Tanzania,
Nd. John Ulanga, Katibu Mkuu TFF, Nd. Kidao Wilfred, Mwenyekiti wa bodi ya Ligi
Kuu, Nd. Steven Mnguto na Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Nd. Boniface Wambura,
Pamoja na Wakurugenzi wa Bodi na wafanyakazi Benki ya KCB Tanzania.
Akizungumza na waandishi
wa habari wakati wa kusainiwa mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB
Tanzania, Nd. Cosmas Kimario alisema kwamba pamoja na dhamira ya benki hiyo
kurudisha kwa jamii, udhamini huo pia ni fursa kubwa kwa Benki ya KCB kuwekeza
kwenye sekta yenye kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa kukuza ajira na vipaji vya
vijana wa Kitanzania.
Zaidi ya kutengeneza
ajira kwenye soka, Benki hiyo imewekeza kwenye programu ya KCB 2jiajiri ambayo
hadi sasa imetoa mafunzo ya uweledi wa biashara kwa wanawake 256 na vijana 100
kuanzia mwezi Oktoba. “Matarajio ya benki yetu ni kuona Watanzania wengi zaidi
wanapata ajira kupitia sekta mbali mbali tunazozigusa.” Alisema Nd. Kimario.
“Sisi Benki ya KCB,
mbali na biashara tunatimiza wajibu wetu
katika jamii inayotuzunguka kwa kuiunga mkono serikali yetu kupinga umasikini
nchini. Hivyo pia tunasaidia jamii hitaji kupitia sekta za: elimu, afya,
mazingira, wajasiriamali, watoto waishio katika mazingira magumu.” Aliongeza
Nd. Kimario.
Rais wa TFF, Nd. Wallace
Karia aliishukuru Benki ya KCB Tanzania kwa kuidhamini Ligi kuu Tanzania Bara
jambo ambalo alisema litasaidia kufanikisha msimu huu wa ligi kuu 2019/20. Pia alizitaka taasisi zingine na watu binafsi
kuiga mfano huo kuweza kutoa michango ya hali na mali ili kukuza maendeleo ya
soka kwa timu za ligi kuu.
No comments:
Post a Comment