Mkuu wa Bidhaa na Huduma kutoka Tigo, David Umoh akimkabidhi Home Internet Router Mtangazaji wa Clouds Tv, Abdallah Kamelo, katika uzinduzi wa huduma ya kwanza na ya kipekee ya Home Internet kutoka Tigo, Katikati ni Afisa Mkuu wa Biashara, Tarik Boudiaf
|
Meneja Huduma za Intaneti Mkumbo Myonga akiwaelezea waandishi wa habari, jinsi gani Mteja anaweza kuangalia salio, kununua kifurushi kwa kupitia Tigo Pesa App katika uzinduzi wa huduma ya kipekee ya Home Internet. |
Dar es Salaam, 3 Septemba 2019: Wateja wa Kampuni ya mawasiliano,Tigo, kwa mara ya kwanza watapata fursa ya kufurahia huduma Home Internet yenye kasi ya 4G+ majumbani mwao.
Huduma hii ni ya kwanza na ya kipekee Tanzania, yenye ubunifu wa hali ya juu itakayowafanya wateja wafurahie intaneti ya 4G+ kwa kutumia vifaa vya Router au Modem.
Kampuni ya simu ya Tigo imezindua rasmi huduma hiyo ambayo itatatua changamoto ambazo watumiaji wa mitandao ya simu hususan wale wa majumbani wamekuwa wakikabiliana nazo.
|
No comments:
Post a Comment