A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, July 20, 2019

Vibarua waliokuwa wakifanya kazi ujenzi wa reli wala shavu serikalini


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa vibarua waliokuwa wakifanya kazi katika  ujenzi wa reli Tanga - Kilimanjaro wapewe ajira na kuwa watumishi.


Waziri Mkuu amesema hayo  wakati wa uzinduzi wa treni ya mizigo ya Tanga - Kilimanjaro baada ya kusimama kwa miaka 12.

“Wale vibarua waliokuwa wakifanya kazi katika  ujenzi wa reli hii, sasa wabadilishwe kutoka kuwa vibarua na kuwa watumishi, wapeni ajira,” Waziri Mkuu.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa amesema kuwa  “Tumeanza na treni ya mizigo, tutairudisha treni ya abiria. Mpaka sasa tumetumia shilingi billioni. 5. 7 kuirudisha njia hii, na wahandisi wazawa ndio wamesimamia zoezi hili lote.”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages