A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, July 20, 2019

Wabunge watatu wajitosa sakala la kina Kinana


Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe, siku chache baada ya kuwavaa Makatibu Wakuu Wastaafu wa CCM, Yusuf Makamba na Abdulrahman Kinana, Wabunge wengine wawili wa chama hicho nao wameibuka wakiwapinga wastaafu hao.

Wiki iliyopita Kinana na Makamba waliandika barua kwa Baraza la Wazee wa CCM, wakitaka chama kichukue hatua dhidi ya mtu anayewachafua, huku akijipambanua kuwa mwanaharakati huru anayepambana na wanaomuhujumu Rais Dk. John Magufuli.

Kutokana na hilo, Bashe alisema waraka huo una malengo ya kugawa chama na kuwataka viongozi hao wastaafu wapambane na mtu huyo bila kuingiza chama kwenye vita yao.

Jana, Mbunge wa Simanjiro, James ole Millya, naye alisema yeye si shabiki wa mwanaharakati huyo, lakini Watanzania watafakari kwa kina taarifa ya wastaafu hao.

“Je, mzee Makamba na Kinana wana uhalali gani wa kisiasa (moral authority) ya kukosoa CCM ya Dk. Magufuli  iliyorudi kwenye misingi iliyoanzishwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kinyume na CCM yao waliyohudumu kwenye vipindi tofauti ambayo dhamira yake ilikuwa ni kuhudumia wachache ambao ni matajiri (mafisadi)?” alihoji Millya.

Akihojiwa na kipindi cha Tuongee Asubuhi cha Star Tv jana, Mbunge wa Geita Mjini, Joseph Msukuma, alisema waraka wa wastaafu hao umewafanya waamini wanazo njama kubwa.

“Ule waraka umetufanya tuamini kumbe yule (Cyprian) Musiba sio kichaa, ni mwanaharakati, anaeleza mpango wa kihuni unaofanywa na hawa wazee.



“Jana niliandika kwenye group la Bunge kuwa uvumilivu una mwisho, huwezi kumwita Rais mshamba na amechanganyikiwa.

“Huo waraka ni wa kijinga, hawa wazee wakiendelea tutawapiga na tutasema uozo wao maana kati ya hao wazee wapo waliokuwa wanaingiza makontena kwa wizi, wamwache Rais, na mimi namshauri Rais asiwasikilize,” alisema Msukuma.

Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde, Leo katika Mkutano wake na waandishi amesema kuwa Waraka wa wazee hao wamepotoka kwa kutoa waraka ambao umewaonyesha ni wanasiasa wazoefu lakini musiba amewaendea kwenye jicho wasiloliona na hawakupaswa kuutoa huo waraka.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages