Mkurugenzi wa
Idara ya Hazina na Masoko ya Fedha wa Benki ya NBC, Peter Nalitolela (kulia)
akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam (UDBS), wakati wa semina kuhusu ujuzi katika sekta ya benki pamoja na
masoko ya fedha na mitaji hapa nchini. Semina hiyo ilifanyika chuoni hapo
jijini Dar es Salaam juzi.
Wakala wa
Mauzo ya Masoko ya Fedha na Mitaji wa Benki ya NBC, Emmanuel Gasirabo
akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam (UDBS), wakati wa semina kuhusu ujuzi katika sekta ya benki pamoja na
Masoko ya fedha na mitaji hapa nchini. Semina hiyo ilifanyika chuoni hapo
jijini Dar es Salaam juzi.
Mkuu Kitengo
cha Mauzo ya Fedha za Kigeni Wateja Wakubwa na Mashirika wa Benki ya NBC,
Juliana Mwapachu akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Biashara ya
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), wakati wa semina kuhusu ujuzi katika sekta
ya benki pamoja na masoko ya fedha na mitaji hapa nchini.Semina hiyo ilifanyika
chuoni hapo jijini Dar es Salaam juzi.
Mkuu wa
Uendeshaji Mizania wa Benki ya NBC Henry Lesika, akizungumza na baadhi ya
wanafunzi wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), wakati
wa semina kuhusu ujuzi katika sekta ya benki pamoja na masoko ya fedha na
mitaji hapa nchini.Semina hiyo ilifanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam
juzi.
Meneja Mikopo
Midogo midogo wa Benki ya NBC, Mtenya Cheya akizungumza na baadhi ya wanafunzi
wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), wakati wa semina
kuhusu ujuzi katika sekta ya benki pamoja na masoko ya fedha na mitaji hapa
nchini. Semina hiyo ilifanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam juzi.
Mmoja wa
wanafunzi wa UDBS akiulizwa swali katika semina hiyo iliyoandaliwa na NBC
ilikiwa na moja ya majukumu ya shughuli za kijamii za benki hiyo.
Mmoja wa
wanafunzi wa UDBS akiulizwa swali katika semina hiyo iliyoandaliwa na NBC
ilikiwa na moja ya majukumu ya shughuli za kijamii za benki hiyo kwa lengo la
kuongeza ufahamu wa wanafunzi hao katika masuala yab sekta za kibenki na masoko
ya fedha na mitaji.
Na Mwandishi Wetu
WATANZANIA
wameshuariwa kuwekeza katika masoko ya fedha ili kunufaika na fursa
zinazopatikana katika masoko hayo ambayo hayahitaji mtaji mkubwa wa kuanzia
imeelezwa.
Ushauri
huo umetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Hazina na Masoko wa Benki ya NBC, Peter
Nalitolela katika warsha maalumu iliyoandaliwa na NBC kwa wanafunzi wa Shule ya
Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), iliyofanyika chuoni hapo, Dar
es Salaam hivi karibuni.
Alisema
lengo kubwa la warsha hiyo ni kunoa uelewa wa wanafunzi hao kuhusu masoko ya
fedha, ili wawe na uwezo wa kuchangamkia fursa lukuki zilizopo sokoni hapo
punde wanapomaliza masomo yao.
“Kuna
kasumba iliyojengeka miongoni mwa watu wenye vipato vya wastani kuwa
kuwekeza katika masoko ya fedha ni ghali na ni eneo la
uwekezaji ambalo limeachiwa matajiri, kitu ambacho hakina ukweli wowote
ukiangalia hali halisi”, alisema mkurugenzi huyo.
Bwana
Nalitolela aliongeza kuwa kiwango cha chini kabisa kinachohitajika kuwekeza
katika soko la fedha ni shilingi sita, fedha ambayo alisema inaweza kupatikana
kwa mtu yeyote aliyejiwekea malengo ya dhati ya kutunza fedha kwa ajili ya
kuwekeza kwa manufaa yake ya baadaye.
Nalitolela
alisema cha kushangaza, watu wengi ambao wanajichukulia kuwa wenye kipato cha
chini wana tabia ya kuwekeza kwenye biashara zilizozoeleka kama kununua
daladala au kufungua duka la rejareja, miradi ambayo kiuhalisia inahitaji mtaji
mkubwa kupindukia ule unaohitajika kuwekeza katika hati fungati, hisa au
dhamana.
“Tunawashauri
watanzania wawekeze kwenye makampuni mengi yaliyobinasishwa na ambayo yanafanya
vizuri kibiashara, ili washiriki katika kuendesha uchumi wao na vilevile
wajizolee sehemu ya faida inayotengenezwa na makampuni hayo,” alisema
Nalitolela.
Aidha kuhusu mafunzo hayo
Nalitolela alisema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya mpango wa NBC kutumia sehemu
ya faida yake kusaidia ustawi wa jamii, na yanalenga kuwapatia wanafunzi
wanaosomea fani za fedha na benki katika Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam stadi za masoko ya fedha ili kuwaanda kuyatumia na kufaidika nayo.
“Haja
hii ndiyo inaleta msukumo wetu wa kuelemisha wanafunzi ili watambue ni jinsi
gani elimu yao ya darasani inahusiana na hali halisi kwenye masoko
ya fedha. Kama mtoaji mkongwe wa huduma za fedha, NBC itaendelea kuhamasisha umma
ili kupanua wigo wa matumizi ya masoko ya fedha.”
No comments:
Post a Comment