A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, June 22, 2019

RC MAKONDA AOKOA MAISHA YA WATOTO 60 ACHANGIA GHARAMA ZA UPASUAJI WA MOYO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimpa pole mtoto Lodric Dalema (2) aliyeletwa hospitali hapo kutoka Katesh, Manyara ambapo alipewa tiba ya ugonjwa wa kifua kikuu kwa zaidi ya miezi 6 kabla ya kugundulika na tatizo hilo na kuletwa JKCI kulia ni mama wa mtoto huyo bi. Paulina Saktai, leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni  ishirini mmoja ya wazazi wa watoto wenye matatizo hayo bi. Agnes Mahenge pesa zilizotolewa na ukoo wa Samaj Brotherhood ili kusaidia kufanikisha  upasuaji kwa watoto 10, utakaoanza jumatatu wiki ijayo, leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni  ishirini kutoka kwa mwenyekiti wa ukoo wa Samaj Brotherhood Harish patel ambazo wamechangia kusaidia kufanikisha  upasuaji kwa watoto 10, utakaoanza jumatatu wiki ijayo, leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wazazi na watoto wenye matatizo ya moyo pamoja na ukoo wa Samaj Brotherhood na wafanyakazi wa taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es Salaam.

Awaomba wadau, mashirika na makampuni kujitolea kuokoa maisha ya watoto hao, awapongeza Samaj Brotherhood kwa kusaidia watoto hao.

ZAIDI ya  wagonjwa laki tatu wenye matatizo ya moyo wameonwa na madaktari bingwa wa moyo tangu kuanzisha kwa taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) mwaka 2015 na zaidi ya wagonjwa 3000 kufanyiwa upasuaji ukilinganisha kasi ya upelekaji wa wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu ambapo kwa mwaka wagonjwa kati ya 50 hadi 100 pekee ndio waliokuwa wanafanikiwa kupelekwa nje kwa matibabu.

Akizungumza katika hafla ya kupokea fedha za matibabu takribani shilingi milioni 20 zilizotolewa na ukoo wa Samaj Brotherhood Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa mahitaji kwa watoto hao ni makubwa sana na zaidi ya watoto 500 wanahitaji kufanyiwa upasuaji hadi kufikia sasa na amewaomba watanzania, wadau na mashirika mbalimbali kuwagusa watoto hao kwa namna moja au nyingine ili kuweza kuokoa maisha yao.

Makonda amehaidi kusaidia kwa kuchangia gharama za upasuaji kwa watoto 60 kuanzia mwezi Julai hadi Desemba mwaka huu na kuahidi kuwa huduma muhimu za namna hiyo ikiwemo afya zinazidi kuletwa karibu zaidi na wananchi.

Aidha RC Makonda amemshukuru Rais Dkt. John Magufuli kwa  kuwezesha uwepo wa kituo hicho cha moyo na amewapongeza na kuwashukuru wana ukoo wa Samaj Brotherhood kwa kuendelea kuwa wadau na washiriki bora katika kusaidia jamii hasa watoto katika sekta ya afya.

Kwa upande wake mwenyekiti wa ukoo wa Samaj, Harish Patel amesema kuwa serikali itoe elimu ya utambuzi hasa katika maeneo ya vijijini na Wilayani ambako kuna madaktari bingwa wachache wa matatizo hayo huku akitolea mifano wa watoto waliokuwa wanapewa tiba za magonjwa tofauti na yale waliyokuwa wanasumbuliwa nayo.

Harish amesema kuwa taasisi hiyo ya Hindu imesaidia na itaendelea kushiriki katika kusaidia watoto wasio na uwezo katika sekta ya afya pamoja na kushiriki katika sekta za madini, michezo, afya, elimu na kilimo.

Awali akieleza namna taasisi hiyo inavyofanya kazi Mkurugenzi wa taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa. Mohamed Janabi amesema kuwa taasisi hiyo inaongoza kwa kufanya upasuaji kwa idadi kubwa barani Afrika ukiitoa Afrika kusini ambapo kwa mwaka jana pekee jumla ya idadi za upasuaji zilizofanyika ni 1352.

Janabi amesema kuwa taasisi hiyo imepunguza kwa kiasi kikubwa gharama na idadi  ya wagonjwa waliokuwa wanapelekwa nje ya nchi kwa matibabu huku akieleza kuwa kwa mwaka 2015-2018 idadi za upasuaji zilizofanywa na taasisi hiyo ni zimekuwa na matokeo chanya.

Amesema kuwa kati ya watoto 100 wanaozaliwa mtoto mmoja ana tatizo la moyo na kwa makadirio kwa mwaka watoto milioni 2 huzaliwa na wao kama taasisi wamejipanga na wataendelea kuwahudumia na kuokoa maisha ya watoto hao ambao kulingana na matatizo yao hufanyiwa upasuaji huo kwa kupasuliwa vifua na wengine hufanyiwa upasuaji wa tundu dogo.

Upasuaji kwa watoto 10 uliofadhiliwa na ukoo wa Samaj Brotherhood utaanza jumatatu wiki ijayo na kuanzia mwezi Julai hadi Disemba watoto 10 waliofadhiliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda watafanyiwa upasuaji.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages