A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, April 10, 2019

FEMATA WAANZISHA SACCOS YAO

IMG-20190410-WA0038
Mchungaji Solomon Ihare Mabati, akiongoza sala ya wachimbaji wa madini kumuombea dua ya afya njema na kuishi maisha marefu kwa Rais John Magufuli.
IMG-20190410-WA0039
Mwenyekiti wa Marema Tawi la Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Shwaibu Mushi akizungumza juu ya wachimbaji wadogo kusajili majina ya wafanyakazi wao.
IMG-20190410-WA0040
Katibu wa Femata Saccos Dk Bernard Joseph akizungumzia mikakati ya wachimbaji kufanya kazi zao kwa usalama ikiwemo katazo la mchimbaji kutozamia mgodini akiwa amelewa.
…………………………………………………………………………………….
SHIRIKISHO la vyama vya wachimbaji madini nchini (Femata) imeanzisha Saccos yao kwa lengo la kujijenga kiuchumi ili wawe na benki ya wachimbaji wa madini Tanzania. 
Katibu mkuu wa Femata, Lister Festo Balegele akizungumza baada ya kikao cha Kamati Tendaji kufanyika mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, kikiongozwa na Rais wa Femata John Bina na bodi ya wadhamini alisema kuanzishwa Saccos hiyo ni hatua mojawapo ya maendeleo kwa shirikisho hilo. 

Balegele alisema kilio cha wachimbaji madini nchini kitatatuliwa baada ya kuanzishwa kwa taasisi hizo za fedha ikiwemo Saccos hiyo na kisha benki ya wachimbaji madini wa Tanzania itakapofuata. 

Aliwataja viongozi wa Saccos hiyo ya Femata kuwa ni Mwenyekiti Money Yousuph, Makamu Mwenyekiti Flora Rashid na katibu mkuu Dk Bernard Joseph. 

Aliwataja wajumbe wa bodi ya Saccos hiyo ni David Bita wa Mara, Doreen Kissia wa Simiyu, Alice Kyanila wa Shinyanga, Mary James wa Mara, Peter Bhene, Lillian Faustine na Shija Lupimo wa Mwanza. 

Mwenyekiti wa Femata Saccos, Money Yousuph alisema uanzishwaji wa Saccos hiyo ni ukombozi kwa wachimbaji madini nchini, ikiwemo kuweza kupata vifaa vya uchimbaji madini. 

Money alisema mchimbaji madini wa Tanzania hivi sasa atakuwa na chombo au taasisi ya kukopa na uwezeshaji wa vifaa na zana za uchimbaji katika mazingira rafiki tofauti na awali. 

Alisema lengo la Rais John Magufuli kuona wachimbaji madini nchini wananufaika na rasilimali yao linakwenda kutimia baada ya mpango wa Saccos kufanikiwa kisha kuanzisha benki ya wachimbaji madini wa Tanzania.
 
Mchimbaji wa madini ya Tanzanite, Rachel Njau aliwapongeza wajumbe wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine ya uanzishwaji wa Saccos hiyo itakayowanufaisha wachimbaji madini nchini.
 
“Tunampongeza mjumbe mwenzetu Flora Rashid ambaye alikuwa na maono na wazo hilo la uanzishwaji wa Femata Saccos ambayo mwisho wa siku limefanikiwa kwa kikamilifu,” alisema Njau. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages