A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, April 10, 2019

aendeleo Hayapimwi kwa kuongeza idadi ya Mikoa

4
Na.Mwandishi Wetu-MAELEZO.
Dhana ya maendeleo inachukuliwa kwa mtazamo wa kawaida kwamba ni kupiga hata kutoka kwenye hali isiyoridhisha na kuelekea kwenye hali yenye unafuu iwe kiuchumi kisiasa kijamii na hata kiutamaduni.
Wapo baadhi ya wasomi na wana falsafa mbalimbali duniani ambao kwa namna moja ama nyingine wamepingana kwa hoja na hata fikra kuhusiana na suala zima na nini maana ya maendeleo lakini pia hata kama nchi ikiitwa imeendelea ni viashiria vipi ambavyo vinatumika kuonyesha maendeleo hayo.
Hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwa katika ziara ya mikoa ya Kusini, kwenye uzinduzi wa barabara ya Namtumbo-Kilimasera-Matemanga -Tunduru Rais Magufuli aliwakumbusha watanzania kuwa wingi wa mikoa ama wilaya sio kiashiria cha kuwa na maendeleo.
Hii ilitokana na baadhi ya wananchi kunyanyua mabango yenye ujumbe wa kutaka wapatiwe mkoa, Rais Magufuli aliwaambia wananchi hao kuwa katika kipindi cha utawala wake hana mpango wa kuongeza idadi ya mikoa na badala yake atahakikisha miradi ya maendeleo kwaajili ya watanzania inakamilika ili hatimaye wawe na maisha bora.
Kwakuwa adhma ya serikali ya awau ya Tano ni kuwatumikia wananchi kwa kutatua changamoto za miundombinu ya barabara, afya maji elimu na kilimo ni vyema ikaeleweka kwamba hayo yote hayahitaji ofisi ya mkuu wa mkoka ili kutekelezeka.
Ni dhahiri baadhi ya wananchi ambao kwa kutokujua waliamua kunyanyua mababgo kwaaajili ya kudai mkoa kwamba, hawaijui dhana nzima ya maendeleo na nini maana yake hasa katika kipindi hiki, kwa hali ya kawaida walipaswa kutambua kuwa barabara za lami walizojengewa ni muhimu sana kuliko ofisi ya mkuu wa mkoaa, pia zahanati vituo vya afya na kusogezwa kwa huduma za maji kadhalika ni muhimu sana kuliko majengo ya ofisi ya mkoa.
Huenda baadhi ya watu bado hawajaielewa dhamira njema ya Rais Magufuli, na ni jambo la ajabu kwa mwananchi ambaye hana huduma za uhakika za afya kuanza kudai kuwepo kwa mkoa, kwakua suala la maendeleo ni kupiga hata kutoka hali duni kwenda kwenye uafadhali ni vyema watanzania wenzetu wakaelewa kwamba kuwepo kwa mkoa hakutasaidia kupatikana kwa huduma za afya, maji hmiundombinu na hata madawa kwenye vituo vay afya.
Katika hili viongozi wa kisiasa ambao ndio wanaoshinikiza uwepo wa mkoa kwa maslahi yao binafsi, ni bora wakajipima kama kweli wanawatendea haki wananchi wao, haiingii akilini kwa wakulima embao hawana uhakika wa masoko kudai kupewa mkoa badala ya kuomba upatikanaji wa solo la uhakika, na pia kwa hali ya kawaida ni jambo la ajabu sana kwa mtu mwenye njaa kuacha kudai chakula badala yake akataka apewe usafiri ama kitu chochote badala ya kutibu njaa yake kwanza.
Ni dhahiri kwamba watanzania hasa wa maeneo ya vijijini bado hawajatambua jitihada kubwa zinazofanywa na Rais Magufuli katika kuwaletea maendeleo, ni vyema viongozi wa kisiasa wakajua uelekeo wa Serikali ya awamu ya Tano ambayo lengo lake kuu ni kuona watanzania wanapata unafuu wa maisha kwa kutumia rasilimali zilizopo kwani kwa kipindi kirefu zimekuwa zikiwanufaisha watu wachache hasa wale wenye uchu wa madaraka na kujilimbikizia mali.
Miradi mingi mikubwa ya kuishangaza dunia inaendelea mfano ujenzi wa reli ya kisasa ya standard gauge, ununuzi wa ndege mpya, ujenzi wa viwanja vya ndege, ununuzi wa meli na vivuko pamoja na ujenzi wa barabara na viwanda mbalimbali nchi nzima, haya yote yanawezekana kwakuwa watanzania wameamua kufanya kazi na pia kulipa kodi.
Kwa kuyatambua hayo tunaungana na Rais Magufuli kwa kuwaambia baadhi ya watanzania wenzetu kuwa maendeleo sio kuongezeka kwa idadi ya mikoa wala wilaya bali kuimarika kwa huduma muhimu za kijamii na kiuchumi zinazowezesha wananchi hasa wa hali ya chini kufurahia matunda ya rasilimali ambazo Taifa hili limejaliwa.Tuendelee pia kujivunia na kulinda Amani yeti kwani ni tunu ambayo mataifa menig wameipoteza ka kwa hali ya kawaida kurudi kwake haiwezekani

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages