
Meneja Masoko wa StarTimes Tanzania, Bw. David Malisa,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)

Muhamasishaji wa Mtandaoni Wema Sepetu akikikabidhi zawadi kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Mapambano kwa niaba ya StarTimes Tanzania

Muhamasishaji wa Mtandaoni Dinah Marious akikikabidhi zawadi kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Mapambano kwa niaba ya StarTimes Tanzania

Timu ya Idara ya Masoko StarTimes Tanzania na Wahamashaji wa Mtandaoni Dina Marious na Wema Sepetu wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa
Shule ya Msingi Mapambano ya Jijini Dar es Salaam
…………………..
Kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes imetangaza ujio wa chaneli ya watoto kwa lugha ya Kiswahili kupitia king’amuzi chake. Chaneli ya StarTimes Kids itakuwa na chaguo la lugha ya Kiswahili kuanzia tarehe 10 Aprili mwaka huu.
Chaneli ya ST Kids ni mahususi kwa ajili ya watoto wadogo wenye umri kati ya 5 hadi 9, maudhui yake yanalenga kuwajengea watoto uwezo wa kuwa wabunifu na kuhusiana vizuri na wazazi wao.
“Kwa kuonyesha tunajali ukuaji wa mtoto pamoja na utamaduni wa kitanzania, kwa sababu lugha ni sehemu ya utamaduni basi kuwa na vipindi vya watoto katika lugha ya Kiswahili itawasaidia kuwajengea kujiamini na kujifunza kwa urahisi zaidi kwa sababu ni lugha ambayo wanaielewa” Zamaradi Nzowa, Meneja Maudhui StarTimes Tanzania
Hii ni chaneli ya kwanza ya watoto Tanzania ambayo vipindi vyake vitakuwa katika lugha ya Kiswahili hivyo ni nafasi ya kipekee kwa wazazi kuwapatia watoto wao kilicho bora kwa ajili ya ukuaji bora.
“Katuni ambazo zitakuwa katika lugha ya Kiswahili ni pamoja na Bonnie Bears, Jingju Cat (Paka wa Opera), Forest Frenzy of Bonnie Bear na Foolish Wolf and his Friends. Vipindi vitaanza kuoneka saa 12 jioni hadi saa 2 Usiku na vitakuwa vikiwa vikurudiwa kwa muda mbali mbali”. Aliongeza
Mbali na katuni kutakuwa na vipindi vingine vitakavyokuwa vikifundisha watoto mambo mbali mbali kama michezo, kuchora, kutengeneza maumbo pamoja na nyimbo.
Katuni na vipindi vingine vya Kiswahili vitaanza kuonekana saa 12 jioni siku ya tarehe 10 Aprili kwenye chaneli ya ST Kids ambayo inapatika katika kifurushi cha MAMBO kwa watumiaji wa dikoda za Antenna na kifurushi cha SMART kwa watumiaji wa dikoda za Dish nchi nzima.
“Vile vile chaneli ya ST Kids inapatikana katika kifurushi cha UHURU kilichoboreshwa zaidi katika msimu huu wa siku kuu ya Pasaka. Awali kifurushi cha UHURU kilikuwa kikigharimu Tsh 24,000 ila kwa sasa kinapatikana kwa Tsh 18,000 pekee. Mteja atapata chaneli zote”. David Malisa, Meneja Masoko StarTimes Tanzania
“Hivyo wazazi wasipoteze nafasi hii ya kipekee kuwafurahisha watoto wao katika msimu huu wa siku kuu, lakini pia nafasi ya wao kufurahia maudhui mengine kama Waaris, Asintado pamoja na ligi ya Europa inayoendelea tena Alhamisi hii”.
No comments:
Post a Comment