A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, February 19, 2019

Waziri Mkuu amsimamisha kazi mweka hazina Kibondo

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mweka Hazina wa Halmashauri ya wilaya ya Kibondo, Thomas Chogolo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma  zinazomkabili za ubadhilifu wa makusanyo ya mapato ya halmashauri hiyo.

 Pia, Waziri Mkuu amewataka watendaji wa halmashauri huyo kumaliza haraka migogoro yao ya kiutendaji kabla ya Serikali haijawachukulia hatua kwani wanachokifanya ni kinyume na maelekezo yake.

Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo leo  wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Kigoma.

 “Katika Serikali hii suala la ukusanyaji wa mapato ni jambo nyeti na limepewa kipaumbele, hivyo ni lazima fedha inayokusanywa itumike kama ilivyokusudiwa ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi.”

 Waziri Mkuu amesema wananchi wa halmashauri hiyo wanalipa kodi kupitia kwa watendaji wa kata katika maeneo yao lakini  Mweka Hazina haingizi kwenye mfumo wa Serikali. Mbali na fedha za makusanyo ya kodi pia matumizi ya fedha mbalimbali zinazopelekwa na Serikali katika halmashauri hiyo nayo hayaridhizishi. Ametoa mfano wa fedha za sekta ya Afya ambapo zaidi ya bilioni mbili zimepelekwa na dawa hakuna.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages