A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, February 19, 2019

Waziri Makamba aelezea hali ya Ruge Mutahaba

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano, January Makamba
amesema alipata nafasi ya kwenda Afrika Kusini kumuona Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi
Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Clouds 360 kinachoruka Clouds TV ambapo ameeleza
Madaktari wanaomtibu Ruge wamempa jina la mpambanaji kutokana na namna anavyoumwa.

"Mimi nilipata nafasi ya kwenda South Afrika, nikaamua nikawaone madaktari wake, wamempa
jina wanamuita 'RUGE THE FIGHTER," amesema Waziri Makamba.

Katika hatua nyingine, amesema Sheria ya Makosa ya Mitandao ya Mwaka 2015, hakuhusika katika mchakato wa utungwaji kwa sababu alikuwa Naibu Waziri Mawasiliano, na mchakato ulihusisha wataalamu wa wizara, makatibu wakuu, mawaziri, na yeye hakuwa miongoni mwa makundi hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages