Klabu ya Simba SC ilitamani mechi yao dhidi ya Al Ahly ichezwe saa nane mchana kwenye jua kali lakini Caf imewapiga ‘stop’.
Ahly wanapokuwa nyumbani dhidi ya timu za Afrika Mashariki, hupanga mechi zao usiku wenye baridi kali ili kuwa katika mazingira mazuri ya kumvuruga mpinzani na kupata matokeo kirahisi.
Mwekezaji wa Simba Mohammed Dewji alisema kwamba; “Najua mnamaanisha nini, lakini kwa sasa haiwezekani, huwa kuna muda maalum ambao unapangwa kabla mashindano hayajaanza na mnakubaliana.”
“Kwa hiyo Caf wanaelekeza mechi zianze saa 10 kwa muda wa hapa, kinachoweza kufanyika ni kusogeza mbele muda ule lakini huwezi kurudisha nyuma ucheze saa 8,” alisema MO huku akicheka na kusisitiza kwamba anajua nia ya Wanasimba wengi.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Monday, February 11, 2019
Simba SC yapigwa 'STOP' na CAF
Tags
MICHEZO#
Share This
About kilole mzee
MICHEZO
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment