Tanzania imepoteza nafasi yake kama taifa lililokuwa linaongoza zaidi katika demokrasia katika eneo la Afrika Mashariki na inafahamika hivi sasa inashindana na maeneo yenye hali ya hatari kisiasa duniani, ripoti mpya imesema.
Gazeti la “The Citizen” linalochapishwa nchini limeandika kuwa Kenya imeipiku Tanzania.
Tanzania imeshuka daraja saba kwa mwaka mmoja uliopita , na kupata jumla ya alama 45 tofauti na utafiti wa 2018 ulioipa alama 53 ambapo ilikuwa inaongoza katika demokrasia kuliko mataifa mengine ya Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC.
Lakini 'Ripoti hiyo Freedom in the World Report 2019' iliyotolewa siku ya Ijumaa inaonyesha kwamba Kenya ndio inayoongoza kidemokrasia miongoni mwa mataifa ya Afrika mashariki.
No comments:
Post a Comment