Januari 29,
2019
Benki yabiasharaya DCBimefanikiwakupatafaidaya
shilingibilioni 1.9katikamwaka 2018
huku ikiipiku hasara ya shilingi bilioni
6.9 iliyopatikana mwaka 2017 ambayo inawakilisha ongezeko la asilimia 463.
Benki imefanya juhudi za makusudi kuhakikisha
inatoka kwenye hasara iliyopata mwaka 2017 na kurudi kwenye faida. Baadhi ya
hatua zilizochukuliwa nikupitia na kuboresha ufanisi wa mfumo wa uendeshaji
biashara ambapo gharama za uendeshaji zimeshuka huku huduma mpya za kidigitali
zimeanzishwa, huduma hizi zimevutia wateja wengi zaidi kufungua akaunti za
amana. Juhudizilizopelekea upatikanaji wa faida mwaka 2018;
1. Mapato
halisi ya ribakuimarika
kutokanana utoaji mikopo katika sekta mbalimbali na kuchangia ongezeko la
mikopo ghafi kutoka shilingi bilioni
88.6 mwaka 2017 hadi bilioni 90.6
mwaka 2018. Mikopo ya jumla ya shilingi bilioni
65 imetolewa mwaka 2018 ambapo kati yake, shilingi bilioni 21 ni mikopo ya wajasiriamali wadogo.
2. Kuboresha ufanisi katika mfumo wa uendeshaji biashara kupitia
mfumo wa kidijitali hukumkazo ukiwekwa katika kuongeza amana za gharama nafuu
kupitia bidhaa za amana za kidijiti na usimamizi wa mizania wenye ufanisi.Gharama za amana zimeshuka kutoka
shilingi bilioni 9.8mwaka 2017
kufikia shilingi bilioni 6.8 mwaka
2018.
3. Kuongeza kasi
ya ukusanyaji madeni yatokanayo na mikopo chechefu na hivyo kupunguza tengo
la mikopo chechefu kutoka shilingi bilioni
4.5 hadi shilingi milioni 263
4. Kuongeza mkazo katika ufanisi wa utendaji na kuchangia upunguaji wa gharama za
uendeshaji kutoka bilioni 21.2 mwaka
2017 kufikia shilingi bilioni 16.9
mwaka 2018
Uboreshaji
huduma na mahusiano ya wateja umekuwa ndio
kigezo kikuu katika kuongeza amana nafuu na za muda mrefu hasa kutoka kwa
wanahisa waanzilishi na mashirika mbalimbali yaliyoendelea kuwekeza na benki ya
DCB.
Huduma za
kidigitalizimekuwa chachu ya kuongeza ufanisi na
kupunguza gharama za uendeshaji na gharama za riba. Hizi ni mathalaniakaunti ya
kidijiti (DCB Digital Account), DCB Kibubu Digital Account, DCB FDR Digital
account. Account hizi zinamuwezesha mteja kufungua akaunti na kufanya miamala
yote ya kibenki, Kutunza pesa na kuwekeza kwa kutumia simu yake ya mkononi.
Idadi ya
wateja imeongezeka kutoka 144,475 mwaka 2017 kufikia 175,204 mwaka 2018 na hivyo kuchangia
ongezeko kubwa la miamala ya kibenki ambapo mapato yasiyo ya riba kuimarika
katika mwaka 2018.
Benki ya DCB ilianzishwa mwaka 2002 ikiwa kama
Benki ya Jumuiya ya Wananchi “community bank” na Manispaa za Jiji la Dar es
Salaam kufuatia kilio cha wakazi wengi wa Jiji kutokuwa na njia rahisi ya
kupata mitaji midogo midogo ya biashara. Benki ya DCB imekuwa ni benki ya
kwanza kuorodheshwa kwenye Soko la Hisa mwaka 2008, na imeweza kukuza mtandao
wake wa matawi kufikia matawi nane likiwepo tawi la Dodoma, na inatarajia
kuongeza matawi mengine mikoani katika miaka ya mbeleni.
No comments:
Post a Comment