Katibu
wa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Baptist Mdende ambaye alikuwa
mgeni rasmi kwenye maonyesho hayo akiwa kwenye moja ya mashine zilizopo
katika karakana ya uhunzi na uundaji wa vyuma akipata maelezo kutoka kwa
wanafunzi ambao wanajifunza kupata ujuzi wa fani hiyo na kuja
kulitumikia taifa hili hata kuanzisha viwanda vidogo vidogo au kwenda
kufanya kazi kwenye viwanda mbalimbali
Katibu
wa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Baptist Mdende ambaye alikuwa
mgeni rasmi kwenye maonyesho hayo akipata maelezo kutoka chumba cha
kompyuta ambacho nacho kipo chuoni hapo
Katibu
wa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Baptist Mdende ambaye alikuwa
mgeni rasmi kwenye maonyesho hayo akiwa kwenye chumba cha mapishi ambako
wanafunzi wa fani ya upishi huwa wanajifunza kwa vitendo.
Katibu
wa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Baptist Mdende ambaye alikuwa
mgeni rasmi kwenye maonyesho hayo akiwa kwenye karakana ya umeme
Hii ni karakana ya useremala ambayo pia inawaongezea ujuzi wanafunzi wa fani hiyo ikiwa na vifaa vya kisasa kabisa
Na Fredy Mgunda,Iringa.
SHIRIKA
lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania
kupitia chuo cha ufundi VTC Mdabulo kilichopo wilaya ya Mufindi mkoani
Iringa linawasaidia watoto yatima na walio kwenye mazingira magumu kwa
kuwapatia elimu ya ufundi bure.
Akizungumza
Mkurugenzi mtendaji wa R.D.O Fidelis Filipatali alisema kuwa shirika
hilo linawasomesha wanafunzi bure wanatoka katika mazingira magumu na
watoto yatima ili kuwapa elimu itakayowakomba katika maisha.
“Lengo
letu ni kuhakikisha wanafunzi walioshindwa kuendelea na masomo mengine
kwenye vyuo vingine wanapata nafasi katika chuo chetu hiki ambacho
kinagharama nafuu na kinatoa elimu bora ya ufundi ambayo inatamsaidia
huko mbele kwenye maisha yake” alisema Filipatali
Filipatali
alisema kuwa shirika hilo limebeba dhima ya Rural Devolopment
Organization (RDO) kwa kutoa ujuzi endelevu kwa jamii ili kuondokana na
kuwa tegemezi katika maisha na kuishi kwa kujitegemea kutokana na ujuzi
unaopatikana chuoni hapo.
“Chuo
cha ufundi stadi cha RDO VTC na shirika kwa ujumla vinanuia kuinua jamii
kutoka a hali ya chini kiuchumi na kufikia hali nzuri ya kimaisha na
ndio maana tupo huku vijijini ambako ndio kuna wananchi wengi wa hali
hiyo” alisema Filipatali
Lakini
Filipatali alisema kuwa chuo hicho kimelenga kuwapa ujuzi wa muda mfupi
na muda mrefu kwa lengo la kuwasaidia kuendelea kufanya shughuli
nyingine za kimaendeleo.
“Tunatoa
ujuzi kwa njia tofauti tofauti hivyo tunapoona kuwa wanafunzi wanauwezo
wa kujitegemea na wapo tayari kwenda kujitegemea huwa tunawaruhusu ili
kupisha nafasi kwa wanafunzi wengine kupata ujuzi wa kiufundi” alisema
Filipatali
Filipatali
alisema kuwa wanafunzi wawapo chuoni hapo wanajifunza ufundi
bomba,kuchomelea,ufugaji wa ng’ombe,upishi,ushonaji,kilimo,elimu ya
kompyuta useremala,ufundi chuma ufundi uashi na ufundi umeme.
“Sasa
wanafunzi yeyote Yule akitoka hapa katika chuo chetu anaweza kujitegemea
kwa kuwa atakuwa ameshapata ujuzi kwa vitendo anaweza kufanyia kazi
mahali popote pale atakapo amua kuweka makzi yake” alisema Filipatali
Aidha Filipatali alisema kuwa vijana wanatakiwa kujituma kwa kufanya kazi na kuacha kuwa tegemezi katika jamii.Naye
katibu wa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Baptist Mdende amewataka
wananchi kuwapeleka watoto kupata elimu ya ufundi katika chuo hicho
ambacho kinatoa elimu kwa gharama nafuu.
“Haiwezekani
kuwa chuo hiki kipo hapa jimboni kwetu lakini wanafunzi wanaosoma hapa
wanatoka mbali na kuja kuchukua ujuzi huu wakati sisi wazawa tunawaficha
watoto wetu tabia kama hii haikubariki hata kidogo hivyo nawaomba
wananchi na viongozi kuhakikisha vijana wetu wanapata elimu ya ufundi
katika chuo hiki” alisema Mdende
Mdende
alisema kuwa elimu ndio ufunguo wa maisha hivyo aliwashukuru shirika
lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania
kupitia chuo cha ufundi VTC Mdabulo kwa kutoa elimu bure kwa wanafunzi
yatima na wanaishi katika mazingira magumu.
No comments:
Post a Comment