Mwanamuziki
wa Bongo fleva Anayezidi kufanya vizuri hivi sasa Aslay amefunguka na
kusema hana Uhusiano wowote wa kimapenzi na msanii mwenzake Nandy.
Kumekuwa
na maneno mengi mengi ambayo yamekuwa yakisababishwa na ukaribu uliopo
kati ya Nandy na Aslay ambapo mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii
imesemakana kuwa wawili hao ni wapenzi.
Kwenye
Interview aliyofanya Friday Night Live ya East Africa Tv, Aslay
amefunguka na kusema ukaribu aliokuwa nao na Nandy ni wa kikazi tu sio
zaidi ya hapo na amesisitiza kuwa yeye tayari ana mpenzi wake na
familia.
"
Nafikiri watu wanaonifatilia watakuwa wanajua kuwa mimi nina mtoto,
kuna mwanamke ambaye nimezaa naye. Nandy nipo naye kwenye kazi zetu za
kimuziki tunazofanya hakuna kingine cha zaidi kinachoendelea kati yangu
na Nandy”.
Nandy
na Aslay wanakimbiza na wimbo wao wa ‘Subalkheri Mpenzi’ ambao
umefikisha zaidi ya viewers milioni tatu YouTube kwa mwezi mmoja lakini
pia wameshawahi kufanya ngoma nyingine iliyofanya vizuri siku za nyuma
iliyoitwa Mahabuba.
No comments:
Post a Comment