Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
Seleman Jafo, akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina elekezi ya maofisa
michezo ilifanyika katika Chuo Cha Mipango cha Dodoma. Semina hiyo
ilihudhuriwa na maofisa michezo wa mikoa kutoka mikoa 26 ikiwemo na
Zanzibar.
Baadhi ya maofisa michezo walioshiriki semina elekezi wakifuatilia hotoba ya Waziri Jafo
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Seleman
Jafo, (Kushoto) akisalimiana na Meneja wa Chapa ya Cola-Cola nchini,
Sialouise Shayo. Wengine pichani ni Maofisa wa Coca-Cola na Maofisa
Michezo.
Maofisa
wa Coca-Cola, Maofisa michezo wakiwa katika picha ya pamoja na Mh.Jafo,
(Katikati wa waliokaa) baada ya ufunguzi wa semina elekezi. Na
Mwandishi Wetu. Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa, Seleman Jafo,ameipongeza kampuni ya Coca-Cola kwa kuwekeza
kudhamini mashindano ya Shule za Sekondari nchini ya UMISSETA kwa
kipindi kingine mwaka huu na kuahidi kuwa serikali nayo pia itaendelea
kuiunga mkono.
Akifungua
semina elekezi ya maofisa wa michezo kutoka mikoa 26 ya hapa nchini
iliyofanyika mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki,ambapo pia aliambatana na
Naibu Waziri wake, Joseph Kakunda, Waziri Jafo, alisema serikali
inatambua mchango mkubwa wa kampuni ya Coca-cola wa kukuza vipaji vya
michezo kwa vijana. “Nimevutiwa sana na maandalizi na usimamizi wa
mashindano ya michezo ya UMMISETA ulivyokuwa mwaka jana,kwa hili
nawashukuru Coca-Cola,nafahamu kuwa mkataba wao ulikuwa wa kudhamini
mashindano haya kuanzia mwaka 2015 hadi 2018,natoa wito kwao kuangalia
uwezekano wa kuongeza muda wa udhamini ikibidi hata kuwa na haki ya
kuyasimamia moja kwa moja,”alisema Jafo.
Pia
alitoa wito kwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuweka mikakati
itakayowezesha vilabu vya michezo vya hapa nchini kukuza vipaji vya
mchezo wa soka vitakavyokuwa vimeibuliwa kupitia mashindano haya na
kuwapatia wachezaji hao nafasi za kuendeleza vipaji vyao. Meneja wa
chapa ya Coca-Cola nchini, Sialouise Shayo alisema “Lengo kuu la kampuni
ya Coca-Cola ni kuwezesha vijana kushiriki katika michezo,kwa mara ya
kwanza pia tutaifikia mikoa ya Tanga na Mtwara ambapo tutatoa jezi na
vifaa vingine vya michezo” Kwa upande wake, Naibu Waziri wa TAMISEMI,
Joseph Kakunda, alipongeza udhamini wa mashindano haya kutoka Kampuni ya
Coca-Cola “Moja ya changamoto kubwa iliyopo ni jinsi ya kuendeleza
vipaji vya michezo vinavyoibuliwa kupitia mashindano ya UMISSETA. Mrisho
Ngassa, Juma Kaseja, Leodgar Tenga ni baadhi ya wanasoka ambao vipaji
vyao viliibuliwa na mashindano haya”.
Alitoa
wito kwa serikali kuongeza juhudi za kuboresha mashindano ya UMISSETA
ikiwemo kuhakikisha inatoa mafunzo kwa walimu wa michezo mashuleni
sambamba na kuhakikisha kila manispaa nchini inatenga maeneo ya viwanja
vya michezo. Semina elekezi ya makocha na maofisa michezo ilifanyika
katika Chuo Cha Mipango cha Dodoma. Ilihudhuriwa na maofisa michezo wa
mikoa kutoka mikoa 26 ya hapa nchini, ikiwemo Afisa Michezo kutoka
Zanzibar,Mwakilishi kutoka Baraza la Michezo la Taifa,Maafisa Utamaduni
wa Mikoa na Wajumbe wa Sekretarieti ya UMISSETA kitaifa.
Kufanyika
kwa semina hii pia ni uzinduzi rasmi wa mashindano ya UMISSETA 2018
uliofanywa na Waziri Jafo,mashindano haya ngazi ya kitaifa yatafanyika
siku za baadaye katika viwanja vya Chuo cha Ualimu cha Butimba mkoani
Mwanza,na aliahidi kumuomba ,Mh.Rais John Magufuli,kuwa mgeni rasmi
wakati wa uzinduzi wake.
No comments:
Post a Comment