Miss
Tanzania 2006 na Msaanii wa filamu, Wema Sepetu akitoka katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu leo mara baada ya kusomewa mashtaka
yanayomkabiri ya Madawa ya kulevya.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii.
BAADA
ya kesi ya matumizi ya madawa ya kulevya inayomkabili aliyekuwa
mlimbwende wa Tanzania 2006 na msaniiwa filamu hapa nchini, Wema Sepetu
na wenzake watatu kunguruma kwa takribani mwaka mmoja, leo Machi 12,
upande wa mashtaka umefunga ushahidi wao.
Hatua
hiyo imekuja baada ya mashahidi watano wa upande wa mashtaka kumaliza
kutoa ushahidi wao na kuiachia mahakama katika maamuzi.
Baada
ya mahakama kupata taarifa hiyo kutoka kwa Wakili wa serikali,
Constantine Kakula, wakili wa Utetezi, Albert Msando aliiomba mahakama
kuwasilisha hoja zao za kuishawishi mahakama kuwa washtakiwa wote hawana
kesi ya kujibu.
"
Mheshimiwa tunaomba kujenga hoja kwa washtakiwa wote watatu kuwa hawana
kesi ya kujibu kuhusiana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapa na
upande wa mashtaka, amedai Wakili Msando.
Kifuatia
ombi hilo, Hakimu Simba ameutaka upande wa utetezi kuwasilisha hoja zao
Machi 23, mwaka huu na kesi hiyo itatajwa tena Aprili 3, mwaka huu.
Kabla
ya upande wa mashtaka kuifunga kesi yao waliwaita mashahidi wawili
kutoa ushahidi ambao ni, Steven Ndondo mjumbe wa shina namba 39 eneo la
Basihaya na askari D 603 Ditektivu Koplo Robert (31).
Katika
ushahidi wake, Ndondo akiongozwa na Wakili wa Serikali, Costantine
Kakula amedai kuwa Februari 4,2017 saa 10 jioni alipigiwa simu na mtu
asiyemfahamu kuwa anahitajika mtaa wa Nazareti nyumbani kwa Wema kwa
ajili ya kufanya upekuzi.
Amedai
kuwa upekuzi ulianzia jikoni ambapo katika kabati la vyombo ulipatikana
msokoto wa sigara ambayo hakuwa akijua ndani yake kulikuwa na nini, pia
walikuta karatasi inayosadikiwa kuwa inatengenezewa mihadarati Mimi sihifahamu polisi ndiyo walisema Rizla.
Pia
katika chumba cha kihifadhia nguo na viatu vya Wema walikuta kipisi cha
sigara ambacho hakijulikani ni cha sigala ya aina gani.
Katika chumba cha wafanyakazi wa Wema kwenye kabati walikuta ganda la kiberiti ndani yake kukaonekana kipisi cha sigara.
Hata hivyo katika chumba cha kulala cha Wema katika upekuzi huo hawakuona kitu chochote.
Kwa
upande wa Koplo Robert alidai kuwa Februari 4,2018 akiwa ofisini kwake
polisi kati muda wa jioni alipewa Vielelezo msokoto mmoja, vipisi viwili
vya msokoto ambayo vilikuwa ndani ya kiberiti vya majani yanayodhaniwa
kuwa ni bangi.
Baada
ya kukabidhiwa na Inspekta Wille alivihifadhi na kwamba alipewa kwa
ajili ya kuvipeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ambapo Februari 6,2018
alivipeleka na kusajiliwa.
Ameeleza
kuwa baada ya vipeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali vilifanyiwa kazi na
kureshwa polisi kuhifadhiwa na hadi sasa vipo polisi.
Mbali
na Wema, wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ya kutumia dawa za kulevya
ni Angelina Msigwa na Matrida Seleman Abbas kwa pamoja wanakabiliwa na
mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na
kutumia dawa za kulevya.
Inadaiwa
kuwa Februari 4, mwaka huu, katika Makazi ya Wema huko Kunduchi
Ununio washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi
vyenye uzito wa gramu 1.08.
Kwa
upande wa Wema yeye anadaiwa kuwa Februani Mosi, 2017 katika eneo
lisilojulikana jijini Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya
Bangi.
No comments:
Post a Comment