A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, January 31, 2018

Historia kujirudia Yanga Vs Lipuli FC


Historia kujirudia Yanga Vs Lipuli FC
Mechi ya ligi kuu soka Tanzania Bara kati ya Lipuli FC dhidi ya mabingwa watetezi Yanga inatarajiwa kukumbusha mashabiki wa soka historia katika miaka 20 iliyopita.


Historia hiyo ni uwepo wa kocha Amri Said kama kocha mkuu wa klabu ya Lipuli FC ambaye miaka takribani 20 iliyopita alikuwa mchezaji wa timu hiyo kabla ya kujiunga na Simba..

Kwa upande wa Yanga kocha msaidizi wa timu hiyo ni Shadrack Sanjigwa ambaye aliwahi kuichezea timu hiyo kwa mafanikio makubwa hivyo atakuwa anakutana na Amri Said ambaye walikutana akiwa Simba pamoja na Selemani Matola ambaye kwasasa ni kocha msaidizi.

Mchezo huo wa ufunguzi wa mzunguko wa pili wa ligi kuu utachezwa jumamosi kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.

Kwenye msimamo wa ligi timu ya Yanga inashika nafasi ya 3 ikiwa na alama 28 wakati wenyeji wao Lipuli FC wakiwa kwenye nafasi 7 wakiwa na alama 16. Katika mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages