MFUKO wa Pensheni wa PSPF, umezindua ofisi mpya mbili moja kisiwani Pemba na nyingine kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza.
Akizungumza
na waandishi wa habari makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam Oktoba
2, 2017, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Mfuko huo, Bi. Laila Maghimbi
alisema, ofisi hizo zimezinduliwa rasmi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho
ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
“Mtakumbuka
kwamba wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba kila mwaka, huadhimishwa wiki ya
huduma kwa wateja duniani, na kwa mwaka huu, Mfuko umzindua ofisi mpya
kule Pemba na Ukerewe ili kuboresha zaidi huduma zetu.”
Akizungumzia mtandao wa PSPF nchini, Bi. Maghimbi alisema, “PSPF ina ofisi kila makao makuu ya mkoa Tanzania Bara na Visiwani.”Bi. Maghimbi alisema, sambamba na ufunguzi wa ofisi mpya,hapa
makao makuu mtaona tunaadhimisha kwa kushirikiana na washirika wetu
kwenye utoaji huduma mbalimbali, ili kuwapatia fursa wananchama wetu ya
kupata huduma kutoka taasisi hizo washirika.
Aliwataja
washirika hao ambao wameweka mabanda ya kutoa huduma kuwa ni pamoja na
Mfuo wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), benki za TPB, NMB, CRDB na Benki
ya Walimu, (MCB).
Alisema,
PSPF katika maadhimisho hayo, inatoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja
na kuwahudumia wastaafu wanaofika kujua mafao yao, pia kusajili
wanachama wapya kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari yaani PSS.Miongoni
mwa wanachama wa PSPF waliofika kupatiwa huduma ni pamoja na Mkuu wa
Mkoa Mstaafu, Dkt. Ibrahim Msengi ambaye alisifu huduma za haraka
zitolewazo na maafisa wa PSPF.
“Kwa
kweli mimi nimeridhishwa na huduma niliyopatiwa hapa, nimefika hapa
kufuatilia malipo ya mirathi ya ndugu yetu, na nimepokelewa vizuri na
kupatiwa huduma stahiki bila ya ucheleweshwaji, hili ni jambo jema na
niwapongeze PSPF kwa uchapakazi wa namna hii.” Alisema.
Wanachama
wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wakihudumiwa kwenye ofisi ya huduma kwa
wateja makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam Oktoba 2, 2017.
Katika kuadhimisha wiki hiyo, PSPF imefungua ofisi nyingine Pemba na
Ukerewe ili kusogeza karibu huduma kwa wanachama wake.
Mwanachama
wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akihudumiwa kwenye ofisi ya huduma kwa
wateja makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam Oktoba 2, 2017.
Katika kuadhimisha wiki hiyo, PSPF imefungua ofisi nyingine Pemba na
Ukerewe ili kusogeza karibu huduma kwa wanachama wake.
Mwanachama
wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akihudumiwa na Bi.Elizabeth Shayo,
(kulia), makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam Oktoba 2, 2017.
Katika kuadhimisha wiki hiyo, PSPF imefungua ofisi nyingine Pemba na
Ukerewe ili kusogeza karibu huduma kwa wanachama wake.
Elizabeth Shayo, (katikati), Afisa Huduma kwa wateja wa PSPF, akitoa maelezo kwa Mwanachama aliyefika kupatiwa huduma.
Afisa
wa Huduma kwa Wateja Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw.
January Iman Buretta, (kushoto), akizungumza na wanachama wa Mfuko huo
waliofika makao makuu kupatiwa huduma Oktoba 2, 2017. Katika kuadhimisha
wiki ya huduma kwa wateja iliyoanza jana, PSPF imefungua ofisi nyingine
Pemba na Ukerewe ili kusogeza karibu huduma kwa wanachama wake.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Fatma
Mkuu
wa Kitengo cha Huduma kwa wateja, Mfuko wa Penshini wa PSPF, Bi. Queen
Edward, (mbele), Meneja Masoko, Mawasiliano na Uhusiano, Bi. Fatma
Elhady, (wapili kulia), na maafisa wa kitengo cha huduma kwa njia ya
simu wakiwahudumia wateja wa Mfuko kwenye kituo hicho.
Mkuu
wa Kitengo cha Huduma kwa wateja, Mfuko wa Penshini wa PSPF, Bi. Queen
Edward, akizungumza na mmoja wa wateja waliofika kupatiwa huduma
Mkuu
wa Mkoa Mstaafu, Dkt. Ibrahim Msengi, (kulia), akipokea nyaraka kutoka
kwa Meneja wa Huduma kwa Wateja, wa Mfuko wa PSPF, Bi. Laila Maghimbi.
Mkuu
wa Mkoa Mstaafu, Dkt. Ibrahim Msengi, (kushoto), akipatiwa maelezo na
Meneja wa Huduma kwa Wateja, wa Mfuko wa PSPF, Bi. Laima Maghimbi.
No comments:
Post a Comment