Airtel
leo wamezindua shamra shamra za wiki ya huduma kwa mteja kwa
kuwakaribisha wateja wake wote waliongia madukani kwao kwa kukata keki
na kuzindua kifurushi maalum cha sh 1000 cha OFA KABAMBE kinachodumu
kwa siku tatu ikiwa ni ishara yakuwashukuru wateja wote nchini.
Akiongea
katika makao makuu ya Airtel Meneja wa Duka la Airtel Bi Celine Njunju
alisema “tunawashukuru wateja na wananchi wote kwa ujumla katika wiki
hii ya huduma kwa wateja inayoanza tarehe 2 hadi tarehe 6 mwezi Oktoba
duniani kote, kwa upendo kabisa Airtel inakupa kifurushi cha OFA KABAMBE
kupitia Airtel Money kitakachokupa uhuru wa kujichagulia kile
unachokipenda kutoka Airtel”.
Ukijiunga
na Ofa kabambe ya Airtel Money, kwa Tshs 1000 tu! utapata GB 2, Dakika
110 za kupiga mitandao yote na SMS bila ya kikomo, huku ukiwa na uhuru
wa kutumia kifurushi hiki ndani ya siku tatu toka pale ulipo nunua.
Alieleza
kuwa “ili kujiunga Piga *150*60# chagua 6 kufurahia vifurushi
vinavyokupa MB na Dakika kibao pamoja na SMS bila ya kikomo”
“uhuru ni wako tumia utakavyo ndani ya siku tatu. alisisitiza Bi Celine
kwa
upande wake Mkurugenzi wa kitengo huduma kwa wateja wa Airtel Bi
Adriana Lyamba alieleza kuwa “ wiki hii huadhimisha kila wiki ya kwanza
ya mwezi oktoba kila mwaka, lakini kwetu Airtel kila siku tunazingatia
swala muhimu la kutoa huduma kwa wateja wetu wote kwa viwango
vinavyotakiwa “Mwaka
huu Airtel tumeipa wiki hii kauli mbiu Building Trust tukimaanisha
kuendelea kuwajengea wateja wote Imani katika huduma tunazotoa” alieleza
Bi Lyamba.
Bi
Lyamba aliendelea kusema “wiki hii pia Airtel tutakuwa na matukio mengi
maalumu kwa wateja wetu lakini muhimu zaidi tunawakaribisha wote
mtembelee katika ofisi zetu za huduma kwa wateja ili muendelee kujipatia
huduma bora kama vile kusajili laini mpya, kujipatia simu na vifaaa vya
mawasiliano original kwa bei nafuu na vitakuwa na ofa kabambe maalum
kwa ajili yako, pia utaelekezwa jinsi yakutumia huduma zetu kama Airtel
Money, Airtel Yatosha, huduma ya kukopa kwa Airtel Money yaani Timiza na
nyingine nyingi
Meneja
wa duka la Airtel Makao Makuu Bi Celine Njuju akiongea na wateja leo
wakati Airtel ilipozindua wiki ya huduma kwa wateja pamoja na kuzindua
kifurushi cha OFA kabambe kinachopatikana kupitia Airtel Money kwa
shilingi 1000 tu na kudumu kwa siku 3. kifurushi hiki pia kinampatia
mteja GB 2, dakika za maongezi 110 kwenda mitandao yote pamoja na sms
bila kikomo uzinduzi wa wiki.
Katikati
ni Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba akikata
keki kuashiria uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja inayoazimishwa
duniani kote kuanzia octoba 2 hadi oktoba 6 huku akiwa amezungukwa na
baadhi ya wafanyakazi wa Airtel pamoja na wateja wa Airtel
waliotembelea duka la Airtel Moroco kujipatia huduma.
Mmoja
kati ya wateja wa Airtel Bw, Kassim Nguya akimlisha keki Mkurugenzi wa
huduma kwa mteja Bi Adriana Lyamba maalum kwa kuashiria uzinduzi wa wiki
ya huduma kwa wateja ambayo huanzimishwa kila mwaka mwezi oktoba tarehe
2 hadi 6. airtel pia imezindua kifurushi cha OFA kabambe ambapo kwa
shilingi 1000 mteja anapata GB 2, dakika za maongezi 110 kwenda
mitandao yote pamoja na sms bila kikomo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Airtel huduma kwa mteja wakiwa tayari kuwakaribisha wateja na kuwahudumia.
Baadhi
ya wateja wa Airtel waliotembelea duka ya Airtel Makao makuu leo
wakilishwa keki na Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel Bi Adriana
Lyamba leo ikiwa ni kusherehekea wiki ya huduma kwa wateja
inayoazimishwa duniani kote kuanzia octoba 2 hadi 6. Airtel mwaka huu
wamesherehekea wiki hio wakiwa na kauli mbiu yao ya BUILDING TRUST yaani
kuwajengea wateja Imani kwa kuwapatia huduma zenye viwango.
No comments:
Post a Comment