Naibu
waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya makazi Mhe. Angelina Mabula
akihutubia katika hafla ya maadhimisho ya 32 ya makazi duniani kutoka
kulia ni mkurugenzi wa nyumba Bw.Pius Tesha na wa pili kulia ni
mkurugenzi wa mipangomiji profesa John Lupala maadhimisho yaliyofanyika
Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi
wa makamu mkuu wa chuo cha ushirika moshi Dkt.Lucas Mataba kulia akitoa
salam kwa Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya makazi Mhe.
Angelina Mabula wa kushoto katika maadhimisho ya makazi duniani
yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano karimjee Jijini Dar es Salaam
leo wa kwanza kushoto ni mkurugenzi wa mipangomiji profesa John Lupala.
mkurugenzi
wa mipangomiji profesa John Lupala kushoto akitoa maelezo kwa wadau wa
nyumba na makazi katika maadhimisho ya 32 ya makazi duniania
yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam kutoka kulia ni Naibu waziri wa
Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya makazi Mhe. Angelina Mabula na wa pili
kushoto ni Mwakilishi wa makamu mkuu wa chuo cha ushirika moshi
Dkt.Lucas Mataba.
Mkurugenzi
msaidizi wa urasimishaji makazi Bi.Beritha Mlonda akiwasilisha makala
ya urasimishaji makazi katika maeneo yaliyoko kwenye mkakati wa mpango
wa makazi bora kwa Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya makazi
Mhe. Angelina Mabula katika maadhimisho ya 32 ya makazi duniani
yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano karimjee Jijini Dar es Salaam
hivi leo.
Wadau
wa nyumba na makazi wakifuatilia mkutano wa maadhimisho ya 32 ya makazi
yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano karimjee Jijini Dar es Salaam
leo ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “sera za nyumba ,nyumba za
gharama nafuu”.
Naibu
waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya makazi Mhe. Angelina Mabula,
kulia ni mkurugenzi wa mipangomiji profesa John Lupala na kushoto ni
Mwakilishi wa makamu mkuu wa chuo cha ushirika moshi Dkt.Lucas Mataba
wakiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa nyumba na makazi wa bodi ya
mwenge Jijini Dar es Salaam katika madhimisho ya 32 ya makazi duniani
yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano karimjee Jijini Dar es Salaam
leo.(picha na paschal dotto- MAELEZO).
………………
Na.Paschal Dotto-MAELEZO .
Serikali
kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imewataka
wananchi kuzingatia Sheria wakati wa ujenzi wa makazi yao ili kuepuka
kujenga kwenye maeneo yasiyoruhusiwa jambo linalosababisha bomoa bomoa
isiyo ya lazima.
Naibu
Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Angelina Mabula aliyasema hayo leo Jijini Dar
es Salaam katika Maadhimisho ya Siku ya Makazi duniani ambayo
yalifanyika katika ukumbi wa Karimjee.
Mhe.Mabula
alisema kuwa ni vyema wananchi wazingatie sheria kabla hawajaanza
kujenga makazi yao husika kwa kutoa taarifa kwenye ofisi husika ili
kuepuka ukiukwaji wa Sheria za nchi katika ujenzi wa makazi.
“Watanzania
tunakumbushwa kuzingatia Sheria na taratibu za nchi kwa sababu ubomoaji
unaofanyika siyo kwa makusudi bali ni kwasababu tu watu wamekiuka
Sheria zilizopo na pengine watumishi wasio waaminifu ndani ya Serikali
ambao wanawapa watu maeneo pasiporuhusiwa”, alisisitiza Mhe. Mabula
Akizungumuzia
mpango mkakati wa Wizara hiyo Mhe. Mabula alisema kuwa zaidi ya Miji 26
nchini ikiwemo Mtwara, Singida Mwanza na Dar es Salaam iko kwenye
mchakato wa kupangilia makazi yake na kuwawezesha wananchi kuondokana na
adha ya msongamano wa makazi.
Aidha
Mhe. Mabula alisema kuwa katika maadhimisho hayo ya 32 yenye kauli mbiu
isemayo ‘Sera za Nyumba :Nyumba za Gharama Nafuu’ ambayo inalenga zaidi
kuimarisha sera za nyumba na makazi kwa kufuata sheria na taratibu kwa
ujenzi wa makazi ya jamii yenye ubora zaidi.
Mhe.Mabula
aliongeza kuwa kwa Sera hii ina madhumuni makubwa katika kuhakikisha
nyumba na makazi bora yenye huduma za msingi kwa jamii toshelezi ,kuwa
na mazingira salama ya kuishi kwa wananchi wote hususani wenye mahitaji
maalum wakiwemo watoto, vijana, wanawake, wazee na watu wenye ulemavu
pamoja na upatikanaji wa usafiri na nishati endelevu zenye gharama nafuu
,ili kuwezesha yote haya ni lazima kujua Sheria inasemaje katika
kupangilia miji iliyosalama kwa manufaa ya wote.
Alibainisha
kuwa huduma nyingine ambazo zinapatikana kwenye makazi yaliyo katika
mpangilio mzuri ni upatikanaji wa maji safi na salama na mfumo mzuri wa
uondoshaji maji taka kwa ajili ya afya ya binadamu pamoja na uwepo wa
hewa safi na ya kutosha.
“Ukienda
kwenye eneo ambalo haliruhusiwi kujengwa lazima wakati ukifika kwa
wenyewe kulitumia watakuondoa tu kwa sababu si eneo sahihi la makazi kwa
hiyo mimi niseme ili kuepuka hii bomoabomoa tusijenge bila kuwa na
kibali maalumu kutoka kwenye taasisi inayohusika ili kuweza kukidhi
matakwa ya sheria na taratibu za makazi salama”,alisema Mhe. Mabula.
Chimbuko
rasmi la maadhimosho ya siku ya makazi duniani lilitokana na Azamio
namba 40/202 la baraza kuu la umoja wa mataifa lililopitishwa
Desemba,1985 na kuanza rasmi mwaka 1986.
No comments:
Post a Comment