Jeshi la Polisi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
leo wametembelea kwenye eneo maalumu lililotengwa kwaajili Showroom zote za
Magari Dar es Salaam Kigamboni kwaajili ya kujionea Maeneo watakayojenga Kituo
cha Polis na Kituo cha Zimamoto.
Upande wa Jeshi la Polisi umewakilishwa na Kaimu
kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Kamanda Benedict Kitalika
ambae amempongeza mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa kuwapatia eneo la kutosha kwaajili ya
kujenga Kituo cha Polisi ili kuhakikisha Ulinzi na Usalama wa Mali zinazoenda
kuwekezwa kwenye eneo hilo unakuwepo.
Amesema Ujenzi wa Kituo cha Polisi Utaanza mara
moja na kuwatoa hofu ya Usalama kwa wale watakaohamishia Showroom katika eneo
hilo.
Kwa upande wake Kamishina Msaidizi wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji Brighton Monyo amesema watahakikisha wanaweka Magari ya
Zimamoto ya Kutosha na Visima vya kutosha kwenye eneo hilo ikikuhakikisha
Majanga ya Moto hayapati nafasi.
Amewahakikishia Usalama wenye Showroom kwakuwa
wamejidhatiti ipasavyo kuhakikisha masuala yote ya kiusalama wa mali zao
yanazingatiwa kwakuwa wataweka vifaa vyote vya kuzima kudhibiti Moto.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
aliagiza wenye Showroom zote zilizopo jijini Dar es Salaam kuhakikisha
zinahamia Kigamboni kwenye eneo maalumu lililotengwa kabla ya Januari Mosi
Mwakani.
No comments:
Post a Comment