Mratibu
wa Ukimwi Mkoa wa Singida Dkt Mohamed Mbalazi akitoa mada katika
mkutano ulijadili uboreshaji wa ushirikiano baina ya serikali na wadau
wa sekta binafsi zinazotoa huduma ya Afya Mkoani Singida.
Afisa
Lishe Mkoa wa Singia Teda Sinde akifafanua jambo katika mkutano
ulijadili uboreshaji wa ushirikiano baina ya serikali na wadau wa sekta
binafsi zinazotoa huduma ya Afya Mkoani Singida.
Mratibu
wa Kifua Kikuu na Ukoma Mkoa wa Singida Dkt Evans Mlay (wa kwanza
kushoto) akipitia dondoo, kabla ya kuwasilisha mada iliyoonyesha mchango
mkubwa wa wadau Sekta ya Afya katika mapambano dhidi ya Kifua Kikuu
Singida, Kulia kwake ni Afisa Mradi wa AMREF Mkoa wa Singida
Donathapeace Kayoza.
Mwakilishi
wa Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Cosmas Sikali akizungumza na wadau wa
sekta binafsi zinazotoa huduma katika Mkoa wa Singida.
Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Salum Manyatta akisikiliza kwa makini maoni
na michango mbalimbali ya wadau ambao ni taasisi na mashirika binafsi
yanayotoa huduma za Afya Mkoani Singida.
Meneja
Mradi wa EGPAF Kanda ya Kati Dkt Joseph Obedi akiandika baadhi ya
mapendekezo ya kuboresha ushirikiano kati ya sekta binafsi na serikali
katika uboreshaji wa huduma za Afya Mkoa wa Singida.
Wadau
mbalimbali wa sekta binafsi wameweza kuongeza nguvu katika kuboresha
sekta ya Afya Mkoani Singida kutokana na ushirikiano mzuri ulipo baina
yao na serikali.
Hayo
yamebainishwa katika mkutano maalumu wa siku mbili uliohitimishwa jana
Mjini Singida, ambapo viongozi wa serikali, taasisi na mashirika 15
yanayotoa huduma za Afya na Ustawi wa jamii Mkoani hapa wamejadiliana
namna ya kuboresha ushirikiano baina yao.
Mratibu
wa Ukimwi Mkoa wa Singida Dkt Mohamed Mbalazi amesema katika mapambano
dhidi ya Ukimwi na Virusi vya Ukimwi (VVU) Mkoani hapa, Sekta binafsi
zimekuwa na mchango mkubwa.
Dkt
Mbalazi amesema wadau hao wameweza kutoa dawa za kupunguza makali ya
VVU, tiba lishe, mafunzo kwa watoa huduma wa afya, ufuatiliaji wa
watumia wa dawa za VVU pamoja na kuandaa takwimu jambo ambalo
limeboresha mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi.
“Sisi
kama watendaji wa serikali tunathamini na kutambua mchango wa wadau wa
sekta afya kwakuwa ni nguzo muhimu sana, mfano wadau wetu shirika la
EGPAF, wametenga bilioni 1.6 kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ukimwi na
maambukizi ya VVU” Mkoani Singida”, amesema na kuongeza kuwa,
“Fedha
hizo zitaongea nguvu pale ambapo kuna changamoto au bajeti inakuwa
haitoshelezi, lakini pia tunaendelea kutoa wito kwa wadua wengine
waendelee kuongea nguvu na wigo wa ushirikiano kwakuwa lengo letu ni
moja yaani kumsaidia mwananchi apate huduma bora za afya”, amesisitiza
Dkt Mbalazi.
Naye
Afisa Lishe Mkoa wa Singida Teda Sinde amesema wadau wamekuwa
watekelezaji wazuri wa masuala ya Lishe Mkoani hapa hasa kwa ngazi ya
jamii hivyo ushirikiano kati yao umekuwa wa manufaa makubwa.Teda amesema
mkutano huo wa wadau umewawezesha watendaji na viongozi wa serikali
kuelewa kwa upana zaidi kazi wanazofanya wadau pamoja na changamoto
wanazopitia ili waweze kusaidiana katika kuboresha hali ya Lishe Mkoani
hapa.
“Mkutano
huu umeongeza na kuboresha ushirikiano baina yetu na wadau wetu ambao
wengi wao wanatoa chakula lishe na elimu ya lishe kwa akina mama
wajawazito, watoto wenye umri wa miezi sita mpaka 59 na akina mama
wanaonyonyesha watoto chini ya miezi sita”, ameeleza Teda.
Ameongeza
kuwa mkutano huo umeweza kusaidia katika kupanga mikakati ya utoaji
huduma ili kuepusha wadau wanaotoa huduma ya aina moja kutoelekeza nguvu
katika maeneo yanayofanana au ambayo hayana uhitaji mkubwa kuliko
mengine.
Akifungua
Mkutano huo Mwakilishi wa Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Cosmas Sikali
aliwataka wadau kujadili sera, sheria, kanuni, maeneo ya kipaumbele
katika miradi mbalimbali, mafanikio na changamoto katika utekelezaji wa
mipango mikakati inayosisitiza ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na
binafsi.
Sikali
amesema endapo nguvu hizi kwa pamoja zitaunganishwa na kuratibiwa
vizuri kwa kiasi kikubwa changamoto zilizopo katika sekta ya afya na
ustawi wa jamii pamoja na maradhi kwa wananchi yataweza
kupungua.Ameongeza kuwa serikali peke yake haitaweza kufikia malengo ya
kupunguza vifo vya watoto, akina mama wajawazito na kuweza kudhibiti
magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza, pamoja na kuboresha afya ya
mazingira na kupata maji safi na salama bila kushirikiana na Sekta
binafsi.
Kwa
upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Salum Manyatta amesema
mkutano huo umeshirikisha wadau wote muhimu wanatoa huduma za afya na
ustawi wa jamii mkoa wa Singida.Dkt Manyatta amesema mkutano huo umeweka
malengo na maazimio ya pamoja na wadau wa sekta binafsi ili kuimarisha
sekta ya afya na ustawi wa jamii Mkoani Singida.
No comments:
Post a Comment