Mkurugenzi wa Halmshauri ya Manispaa ya Kinondoni Aron Kagurumjuli |
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, imetiliana saini mikataba miwili ya ujenzi wa barabara yenye thamani ya sh. bilioni 49 na kampuni za ukandarasi za Estim Constructions Company Limited ya hapa nchini na kampuni ya CCEC ya China.
Mstahiki meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh Benjamin Sitta (kushoto), akitia saini Mikataba hiyo. |
Akizun gumza wakati wa hafka ya utilianaji saini mikataba hiyo, jana, Mkurugenzi wa Halmshauri ya Manispaa ya Kinondoni Aron Kagurumjuli, alisema miradi itakayotekelezwa kupitia mikataba hiyo ipo chini ya Mradi wa Kuboresha jiji la Dar es Salaam(DMDP).
Mkurugenzi huyo Amesema, Utekelezaji wa miradi hiyo itakuwa kimafungu ambapo fungu la kwanza lilianza kutekelezwa Desemba mwaka jana huku baadhi ya barabara zilizohusika ni Makumbusho, Nzasa pamoja na Soko la Samaki Msasani .
Amesema MIkataba iliyosainiwa leo inahusisha fungu la pili na la tatu huku fungu la pili litatekelezwa na kampuni ya ukandarasi ya CCEC ikuhusisha barabara za Makanya, Tandale, Kilongawima, Simu 2000 na Tandale Kisiwani.
Aidha amesema Barabara hizo zina jumla ya urefu wa kilomita 10 na thamani ya ujenzi wake ni sh. bilioni 28. Fungu la tatu litatekelezwa na mkandarasi Estim ambapo barabara zitakazo husika ni Ubungo External, Kisukuru, , Kilungile na Korogwe zenye jumla ya urefu wa Kilomita 7.5 ambapo thamani ya ujenzi wake ni sh.bilioni 21.
Kwa upande wa Meya wa Kinondoni, Benjamin Sitta, alisema mikataba iliyosainiwa kupitita DMDP itahusisha pia Halmshauri za Manipaa za Ubungo na Ilala.
Meya Sitta amesema kuwa kwa sababu hiyo barabara zinaingiliana katika manispaa hizo,huku akiweka wazi kuwa barabara zitakazojengwa kupitia miradi hiyo ya DMDP ni za kisasa na viwango vya juu.
Amesema katika fungu la kwanza la ujenzi umefikia asilimisa 80 inatekelezwa na kampuni ya Estimu.
amewataka wakandarasi kumaliza utekelezaji wa miradi hiyo kwa wakati kutokana na umuhimu wa barabara hizo katika jamii.
Amesema kusainiwa kwa mikataba hiyo kunatokana na kasi ya Rais Dk. John Magufuli ambaye amekuwa akiharakisha shughuli za maendeleo na msimamo wake wa kutaka watu wafanya kazi.
No comments:
Post a Comment