Mwandishi
wa Habari wa gazeti la Guardian, Gerald Kitabu akipeana mkono na Waziri
wa Elimu Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako baada ya
kukabidhiwa tuzo ya mshindi wa kwanza kwenye kuandika na kuelimisha umma
kuhusu matumizi ya sayansi, Teknolojia na ubunifu hususani
Bioteknolojia katika kuendeleza kilimo katika hafla iliyofanyika jijini
Dar es Salaam juzi. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi
na Teknolojia (COSTECH), Dk. Hassan Mshinda
Washindi wa tuzo hizi wakisubiri kutangazwa.
Wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Jim Yonaz akitoa hutuba katika hafla hiyo.
Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Philbert Nyindondi akielezea tuzo hizo
Mkurugenzi Mkuu wa COTECH, Dk.Hassan Mshinda akizungumzia tuzo hizo
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dk.Ayoub Rioba akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mshindi wa tuzo hizo kutoka mkoani Kagera, Benson Eustace wa Clouds Media kikabidhiwa cheti chake.
Mhariri
Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Jim Yonaz
akikabidhiwa cheti kutokana na mchango mkubwa wa vyombo hivyo katika
kuandika habari za sayansi.
Mwakilishi wa TBC, akikabidhiwa cheti kutokana na mchango wa kuandika habari za sayansi.
Ofisa
Mawasiliano wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha SUA ambaye pia ni Mkurugenzi wa
Taasisi ya Elimu Kujiendeleza (ICE), Bujaga Inzengo Kadago akipokea
cheti kutokana na mchango wa vyombo vya habari vya chuo hicho wa
kuandika habari hizo.
Mwanahabari wa gazeti la Habari Leo, Lucy Ngowi akikabidhiwa cheti.
Mwanahabari Hellen Kwavava akikabidhiwa cheti.
Mwanahabari wa Gazeti la Nipashe mkoani Kagera, Restuta Damian akipokea cheti.
Mwanahabari wa gazeti la Guardian, Daniel Simbei akipokea cheti.
Mwanahabari Calvin Gwabara kutoka SUA akipokea cheti.
Mwanahabari wa gazeti la Daily News, Fatma Abdul akipokea cheti.
Mwanahabari Elias Msuya wa Gazeti la Mwananchi akikabidhiwa cheti.
Mwanahabari wa RFA kutoka Mwanza, Coleta Makulwa akipokea cheti
Mwanahabri Dino Mugunde wa Star TV Mwanza akipokea cheti.
Mshindi wa kwanza wa tuzo hizo, Gerald Kitabu akitoa shukurani zake.
Mwanahabari Calvin Gwabara kutoka SUA, akipongezwa na dada yake huku akionesha vyeti vyake.
Na Dotto Mwaibale
WAZIRI
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewataka
waandishi wa habari nchini kutumia taaluma zao kuelimisha jamii kuhusu
habari za sayansi na teknolojia ili kuleta maendeleo nchini.
Akizungumza
wakati wa utoaji tuzo za umahiri katika uandishi wa habari za Sayansi
zilizoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknlojia (COSTECH) kwa
kushirikiana na Jukwaa la Bioteknojia (OFAB), Waziri Ndalichako alisema
tuzo hizo iwe ni chachu za kuandika habari za sayansi kwa undani ili
kuwajengea uelewa wananchi wa.kawaida.
Alisema
ufundi wa waandishi katika.kuandika habari za sayansi utasaidia
kutangaza ubunifu na kuongeza tija thamani katika teknolojia
mbalimbali."Wananchi wanahitaji teknolojia za kisasa katika kurahisisha
utendaji kazi hivyo uandishi wenu utasaidia kuinua sekta ya kilimo na
mifugo ambayo ndio kundi.muhimu katika jamii hasa katika kuelekea uchumi
wa viwanda,"alisema Ndalichako.
Aliwataka
Costech na taasisi nyingine kuendelea kushirikiana na wanahabari
kuelimisha jamii katika masuala ya sayansi.Ndalichako alipongeza COSTECH
na OFAB kwa kuandaa tuzo hizo kwani zitaongeza mori kwa wanahabari wa
kuandika habari za sayansi.
Akielezea
ushiriki wa.waandishi katika shindano hilo lililoanza Januari hadi
Agosti mwaka hii, Mkurugenzi Mkuu wa COTECH, Dk.Hassan Mshinda alisema,
shindano hilo hapa nchini sasa ni mara ya tisa kufanyika na kwa upande
wa Afrika ni la kumi.
Alisema
katika shindano hilo jumla ya makala 200,vipindi vya radio 20 na
televisheni 15 vilishindaniwa.Mshindi alisema watalaam waliobobea ambao
walifanyakazi ya.kutafuta washindi ambao walipata dola 250, 750, 1,000
na 1,500.Kwa upande wake, Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya
Serikali (TSN), Jim Yonaz aliwataka waandishi kuwa daraja kati ya wana
sayansi na jamii.
Alisema
wana sayansi wana lugha ngumu hivyo kupitia waandishi na aina ya
uandishi wao wamesaidia jamii kuelewa habari mbalimbali za
sayansi."Katika kuchangia uchumi wa viwanda waandishi wanakazi kubwa
kuhakikisha wanatoa elimu ya sayansi na kilimo ili kuelimisha
jamii,"alisema Yonaz.
Yonaz
pia aliiomba Serikali kuhakikisha inawawezesha waandishi kwa kuwajengea
uwezo wa ufahamu ili waweze kuelewa zaidi sababu zinazowafanya kuandika
habari mbalimbali.Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dk.Ayoub Rioba alisema,
wana sayansi wana jukumu la kuboresha maisha ya jamii kwa kuhakikisha
wanatumia zana zilizoboreshwa kiteknolojia.Alisema kwa sababu ya lugha
itumikayo na wana sayansi upo umuhimu wa wanahabari kuandika.habari
nyingi za sayansi.
Rioba
pia aliitaka taasisi ya Costech pamoja na taasisi nyingine kuendelea
kufanya kazi za kuelimisha jamii kwa kushirikiana na wana habari ili
kujenga jamii yenye uelewa wa masuala ya sayansi.Miongoni mwa waliopata
tuzo za umahiri wa habari za Sayansi ni pamoja na mshindi wa jumla
Gerald Kitabu (Guardian), Shedrack Sagati(Habari Leo), Elias Msuya
(Mwananchi), Calvin Gwabara, Fatma Abdul (Daily News) na Dino Mugunde.
Wengine ni Lucy Ngowi, Hellen Kwavava, Coleta Makulwa, Daniel Simbei, Benson Eustace na Restuta Damian.
No comments:
Post a Comment