Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Dkt Juliana Pallangyo akizundua mradi huo
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Dkt Juliana Pallangyo
kushoto akipata maelezo ya mradi huo mara baada ya kutembelea kwenye
eneo la mtambo huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mkoani
Tanga,Mhandisi,Robert Gabriel.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Dkt Juliana Pallangyo
akishiriki kucheza ngoma ya wananchi wa Kijiji hicho mara baada ya
kuzinduaa mradi huo
NI ukweli usiopingika utekelezaji wa sekta ya viwanda inahitaji
nishati
ya umeme katika shughuli zake mbalimbali ikiwemo za uzalishaji mali ili
kuweza kupata mafaniko yanayoweza kusaidia kuinua uchumi wao.
Kwani
bila kuwepo kwa nishati hiyo kwa baadhi ya maeneo hasa vijijini kuna
pelekea kushindwa kufikia malengo yao kwa kuongeza uzalishaji wa bidhaa
mbalimbali kwa kuhofia iwapo zitakaa muda mrefu zitaharibika.Licha
ya hivyo lakini pia kukosekana kwa nishati hiyo kuna sababisha
watanzania wenye nia ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo kukwama kufikia
malengo yao waliojiwekea kwa kuvianzisha.
Kufuatia
kuwepo kwa changamoto hiyo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa
Mitaji na Maendeleo (The United Nations Capital Development Fund –UNCDF)
kwa kushirikiana na kampuni ya Ensol Tanzania Limited waliamua
kuanzisha mradi wa umeme wa jua (sola) kwenye kijiji cha Mpale Kata ya
Mpale wilayani Korogwe Mkoani Tanga.
Mradi
huo ambao umekuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Kijiji hicho
umefadhiliwa na Shirika hilo ambao umelenga kuwasaidia kuondokana na
changamoto ambazo zilikuwa zikiwakabili ikiwemo kutumia vibatari wakati
wakienda kujifungua kwenye zahanati ya Kata hiyo.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa mradi huo,Diwani wa Kata ya Mpale Tarafa ya
Bungu wilayani Korogwe Mkoani Tanga,Shemakao Miraji anasema mradi huo ni
faraja kubwa kwa wakazi wa Kijiji hicho na maeneo jirani ikiwemo
kufungua fursa za kiuchumi lakini kuendana sanjari na kauli mbiu ya serikali ya viwanda.
Anasema
awali walikuwa wakilabiliwa na changamoto kubwa ya wakina mama
wajawazito kwenda kujifungulia kwenye zahanati hiyo kwa kutumia vibatari
jambo ambalo lilikuwa ni hatari kwa maisha.
Diwani
huyo anasema faida kubwa za mradi huo utasaidia kuboresha huduma za
afya kwa wakina mama ambao walikuwa wakienda kwenye vituo vya afya kwa
kutumia vibatari lakini baada ya kufika umeme huo utawasaidia kuondokana
na kadhia hiyo ambayo ilikuwa ni hatari kwa maisha yao ambao ni nguvu
kazi kuelekea uchumi wa viwanda.
"Kilio
kikubwa cha wananchi wetu hapa ni maembe yanayoanguka na kuoza ha
hatuwezi kupata namna nyengine ya kuweza kutuepusha na adha ya
kuondokana nayo na hii itatusaidia kuondokana na dhamana hiyo lakini pia
umeme huu utatusaidia kuingia kwen ye uchumi wa kati kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya chai na kukuza zao hilo"Anasema.
Naye
kwa upande wake,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Dkt
Juliana Pallangyo anawapongeza kampuni hiyo na washirika wa kiufundi TTA
kwa juhudi walizofanya kuchagua kijiji hicho kufanya utafiti,kubuni
mradi huo kwa kutafuta fedha na kutafuta taratibu zote katika kutekeleza mradi huo huku akiwataka wananchi kuanzisha viwada vidogo vidogo.
“Katika
kutafuta fedha nafahamu Ensol ilifanikiwa baada ya kushindwa nishwa na
makampuni mengine kwani taasisi hizi zilizotajwa zinatoa fedha kwa
mtindo wa ushindani na wanapokea maombi mengi ya ufadhili kutoka maeneo
mbalimbali ya dunia na Afrika “Anasema
“Lakini
pia nimefurahishwa na zaidi na huduma kadhaa zilizotolewa na mradi kwa
jamii hii hapa kwanza kuwawezesha wananchi kuunganishwa na umeme
ikiwemo kufanyiwa wayaringi kwa mkopo “Anasema.
Anasema
ni kweli katika maeneo ya vijijini huduma ya umeme imefika lakini
wananchi wengi wanashindwa kuunganishwa na umeme kwa sababu gharama ya
kutandaza nyaya kwenye nyumba zao.
“Tunawashukuru
sana Ensol kwa kufikiria kutatua changamoto hii na pia tunawashukuru
Power Africa kwa kuunga mkono jambo hili kwa kutoa fedha na naamini
wananchi wa hapa mpale watatumia fursa ya umeme ambayo sio rahisi
kupatikana kuunganishwa nayo “Anasema.
“Lakini
pia ni kwamba nishati hii ya umeme itapatikana kwa saa 24 kwa siku 7
za wiki bila kukatika hii ni habari njema kwa watumiaji wa umeme kwani
iwapo huduma hiyo itakosekana bado ni changamoto hata maeneo ya mijini
“Anasema.Anasema ni jambo jema kusikia kuwa hapa kwenu masuala ya
mgawo wa umeme kukatika itakuwa ni suala la kusikia kwa wengine na huo
ndio uzuri wa kutumia teknolojia ya umeme wa Jua.
“Pamoja
na hayo lakini niwahamasishe wananchi wa hapa mpale kutumia vizuri
uwepo wa nishati hiyo kwa kuanzisha shughuli za uzalishaji mali ikiwemo
kuanzisha viwanda vidogo vidogo na miradi itakayoweza kuwaingizia fedha
ili kujikwamua kiuchumi”Anasema.
“Msiishie kupata mwanga tu bali tumieni pia fursa hii kuanzisha
biashara
na miradi itakayowaingizia fedha kwani umeme huu unatosha kuanzisha
viwanda vidogo vidogo kama vinu vya kusagia nafaka ,mashine za useremala
na kutengeneza samani “Anasema.
Anasema
kwa kufanya hivyo wananchi wa kijiji hicho watakuwa wameendana
sambamba na mwamko mpya wa Tanzania ya Viwanda ambao utafungua fursa
kubwa za kiuchumi kwao.
Naibu
Katibu huyo anasema kupitia huduma hiyo ni matumaini yake huduma za
afya zitaboreka zaidi kijijini hapo kwani wananchi wengi wa maeneo ya
jirani watakwenda kupata matibabu kwao kutokana na uwepo wa uhakika wa kutibiwa muda wote kunakosababishwa na nishati ya umeme.
“Nawaombeni halmashauri pamoja na serikali ya kijiji kujipanga
kuhakikisha
umeme unaotumika unalipiwa kadri inavyotakiwa kila mwezi kwani
haipendezi kuona nishati hiyo ipo lakini zahanati inakosa huduma hiyo
kwa kushindwa kilipia “Anasema.
“Lakini
pia nikuombe Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe pamoja na uongozi wa
kijiji mjipange hata kwa kutumia fedha mtakazookoa kutoka kwenye
manunuzi ya mafuta ya taa na gesi kwa ajili ya jokofu la madawa muweze
kulipia umeme “Anasema.
“Serikali
sasa kupitia wakala wa Nishati imezindua rasmi mpango wa tatu wa
kusambaza umeme maeneo ya vijijini na tumeweka lengo la kufikia vijiji
vyote ifikapo mwaka 2022.
Naye,
Msimamizi Mkuu wa Mradi huo,Prosper Magali anasema shughuli za mradi
huo zilianza rasmi Machi mwaka 2014 baada ya kutembelea kijiji hicho
pamoja na vyengine vilivyopo wilayani Korogwe.
Anasema
licha ya kutembelea wilaya hiyo lakini pia walitembelea maeneo mengine
Tanzania kutafuta vijiji na maeneo yanayofaa kwa miradi ya uzalishaji
mdogo wa umeme kwa kutumia teknologia ya umeme wa Jua.
Aidha
anaeleza waliamua kuanza mradi wa mfano katika kijiji hicho baada ya
kuwa kijiji bora kwa vigezo walivyoweka vya kiuchumi, kijamii na
kimakjazi ukilinganisha na vyengine walivyotembelea.
“Shughuli
ya mradi zilifuatiwa na zoezi la kufanya upembuzi yakinifu, Mpango wa
kibiashara (Bussines Plan) pamoja na makadirio ya kiufundi mambo ambayo
yalitusaidia kuandaa nyaraka za kuwasilisha kwa wafadhili na wawekezaji
mbalimbali “Anasema.
“Baada
ya hapo mmwaka 2014 mwishoni, Taasisi ya Energy and Environment
Partnership (EEP) Program yenye makao yake makuu huko Pretoria nchini
Afrika kusini inayopata ufadhili wa Serikali za Finland, Uingereza na
Austria kupitia mpango wake wa kutoa ufadhili wa miradi ya nishati
endelevu kwa nchi za kusini na mashariki ya Africa kwa mtindo wa
ushindani “Anasema
“June
10 mwaka 2015 tuliweza kusaini makubaliano rasmi ya EEP ya ufadhili wa
miaka miwili wa mradi huu uliokuwa na thamani ya Euro 263,000 ikiwa ni
asilimia 63 ya gharama za mradi “Anasema.
Anaongeza
kuwa bado wanaendelea na zoezi la kutafuta fedha zaidi za kutekeleza
mradi huo lakini kwa bahati nzuri baada ya mazungumzo ya muda mfupi,
Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo ya Mitaji (United Nations
Capital Development Fund ya UNCDF).
Anaeleza
kufuatia mazungumzo hayo taasisi hiyo ilikubali kutoa asilimia 22 ya
gharama za mradi USD 124,000 na walitiliana saini ya makubaliano ya
ufadhili wa fedha hizo Novemba mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment