Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaizidizi Jonathan Shanna
Warioba, ametoa onyo kali kwa wananchi wenye tabia za udhalilishaji kwa
wanawake kuacha tabia hiyo mara moja huku akisema kwamba udhalilishaji
umesababisha kifo.
Kamanda Shanna amelazimika kusema hayo hayo wakati akizungumza na kituo
hiki akitolea ufafanuzi juu ya tukio la mauaji ya mkazi wa Kijiji cha
Vilabwa Wilaya ya Kisarawe Imma Habibu ( 26).
Kwa mujibu wa Shanna Marehemu aliuwawa juzi majira ya saa mbili asubuhi
wakati walipokuwa kijiweni na wenzake baada ya kutokea ugomvi kati yake
na Ramadhani Habibu (23) ambaye ni ndugu yake, baada ya mwanamke mmoja
ambaye anadaiwa kuwa maumbile makubwa (makalio) kupita, mbele yao.
Alisema baada ya mwanamke huyo kupita mbele yao walianza mabishano
ambapo marehemu alisema mwanamke huyo ana makalio makubwa na Ramadhani
alisema ni makalio ya kawaida na makubwa.
Kamanda Shanna alieleza kuwa baada ya mabishano hayo ndipo ulipozuka
ugomvi hadi kufikia hatua ya Ramadhani kumuua kaka yake kwa kumchoma
kisu kifuani upande wa kulia na kufariki dunia akiwa njiani
anapelekwa hosptali ya kisarawe.
Alisema jeshi la polisi linamshikilia mtuhumiwa kwa kufanya mauaji hayo
na kuwa atafikishwa mahakamani mara moja na kuwa amekubali kuwa
amefanya mauaji hayo.
Kufuatia,tukio hilo kamanda Shanna aliendelea kutoa onyo kwa wananchi
na vijana wanaoshinda vijiweni kuacha tabia ya udhalilishaji hasa kwa
wanawake na kuwa ni kufanya hivyo ni kosa kisheria na kuwa kama kuna mtu
aliyefanyiwa vitendo vya namna hiyo atoe taarifa polisi na atafikishwa
mahakamani.
"Wito kwa wale wanaokiuka haki za binadamu kwa kumdhalilisha mtu waache
mara moja, mfano kisheria hata kumkonyeza mtu ni kosa la jinai hivyo
unapaswa kufika polisi, na tutamfuatilia kisha kumpeleka mahakamani"
Kamanda Shana amefafanua
Pia kamanda Shanna ametoa rai kwa wanawake kuvaa nguo zinazositiri maungo yao ili kuepusha vishawishi na matamanio kwa wanaume
Post Top Ad
Your Ad Spot
Thursday, September 28, 2017
AMUUA KAKAYAKE KISA MAKALIO
Tags
KITAIFA#
Share This
About kilole mzee
KITAIFA
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment