Arusha. Polisi Wilaya ya Arusha imepiga marufuku mikutano ya hadhara ya
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kwa maelezo kuwa kutakuwa na ujio
wa viongozi wa kitaifa jijini hapa.
Pia, kuzuiwa mikutano ya mbunge huyo wa Chadema kunahusishwa na tukio la kuungua moto nyumba za polisi.
Katika barua ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha, Mrakibu Mwandamizi wa
Polisi SSP E.Tille kwenda wa Lema jana Jumatano, imeeleza mikutano yake
imesitishwa.
Mikutano hiyo ilikuwa ifanyike leo Alhamisi na kesho.
Katika barua hiyo, Jeshi la Polisi limeeleza kuwa tarehe ambazo mikutano
hiyo, imepangwa zina mwingiliano na ratiba za shughuli za kiserikali za
viongozi wa juu wa Serikali inayoishia Oktoba 4.
Pia, amesema janga la moto katika kambi ya polisi lililotokea jana usiku
limeleta madhara makubwa hivyo, nguvu kubwa itaelekewa huko.
"Unashauriwa kupanga mikutano yako tarehe yoyote kuanzia Oktoba 5, 2017
pia rejea mazungumzo yangu na wewe ofisini kwangu ya tarehe
29/09/2017," inasomeka barua hiyo.
Hata hivyo, Lema akizungumza na Mwananchi amesema anapinga polisi kuzuia
mikutano yake, kwa kuwa ni ukiukwaji wa sheria na haki za mbunge.
Lema amesema sheria ya Bunge kifungu cha nne fasili ya kwanza,
kinazungumzia uhuru wa mbunge kufanya mikutano jimboni kwake na
kifungu cha 4(1) na (2) vinaelezea uhuru huo wa mbunge kufanya mikutano
na pia ni ukiukwaji wa sheria kuzuia mikutano ya mbunge kwenye jimbo
lake.
Mbunge huyo amesema anaamini, kuzuiwa mikutano yake ni njama kwa kuwa
aawali alipanga kuzungumza na wananchi wa Kata ya Kimandolu ambako
diwani wao amejiuzulu na wananchi wa Mjini Kati.
"Kwanza waliniita wakaniambia hali ya kisiasa si nzuri nisiende kufanya
mkutano Kimandolu kwa kuwa wananchi wanaweza kuwa na hasira baada ya
diwani kujiuzulu, mimi nikawaambia wasiwe na hofu lazima likafanye
mkutano," amesema.
Lema amesema anajua polisi wanaamini atazungumzia sakata la kupigwa
risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na pia ziara ya Rais
John Magufuli ambayo aliifanya hivi karibuni jijini Arusha.
Amesema anashauriana na wanasheria wake kuona kama akubali barua ya polisi au aendelee na mikutano yake.
Hii ni mara ya pili Lema kuzuiwa kufanya mikutano. Agosti 25 alizuiwa
ili kupisha mbio za Mwenge wa Uhuru na mitihani ya darasa la saba na
alitii agizo hilo.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Thursday, September 28, 2017
Lema azuiwa kufanya mikutano
Tags
KITAIFA#
Share This
About kilole mzee
KITAIFA
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment